Kwanini Ukraine haikuomba kuwa sehemu ya USA ili kuepusha huu ujinga unaoendelea sasa?

Kwanini Ukraine haikuomba kuwa sehemu ya USA ili kuepusha huu ujinga unaoendelea sasa?

Mkuu unapotoa hoja, angalia pia jiografia ya eneo unalolitolea mfano!

Yaani ni kama kutolea mfano wa: "kwanini Tz isijiunge na uingereza na kuwa chini ya muungano wa Uingereza?"
Mkuu mbona kuna nchi nyingi tu zimeamua kuwa chini ya himaya fulani yenye nguvu bila kujali jiografia au umbali uliyopo ili kulinda usalama wa sehemu husika. Mfano wa Franch Guiana hii ipo Amerika ya kusini ikipeana mpaka na nchi za Amerika ya kusini kama vile Brazil nk. Kisiwa hiki kimeamua kuwa chini ya himaya ya wafaransa na mpaka leo inatambulika kuwa ni moja kati ya sehemu iliyo chini ya mamlaka ya ufaransa. Kwahiyo hata hawa wa Ukraine wangeyafanya haya zamani, upuuzi huu wa leo usingejitokeza.
 
Kesho utakuja kusema na Zanzibar iwe sehemu ya mmarekani kuepuka unyonyaji wa watu wa bara ktk tanzania
Zanzibar ipo salama salmini chini ya himaya yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Toka kuumbwa kwa dunia hatujawahi kushindwa vita, kuanzia vile vya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika hadi ile ya Uganda na juzi Comoro. So iache iendelee kuwa moja ya sehem yetu na ikiwezekana na Burundi, Rwanda na Malawi pia zijiunge nasi ili ziweze kuwa salama zaidi.
 
Kwan huko ccm akili hizi huwa mnazitumia kumuumiza Mbowe tu na chadema..Kwann hamshaurian kama hiv hapo lumumba.Au gateway ya akil zenu huwa ina change to 127.0.0.1/lumumba😂
Madhara ya kushikiwa akili na mwenyekiti wako ndio haya. Yani inakufanya unakuwa hauko huru kujadili mambo mengine ya maana nje ya box zaidi ya yale anayotaka yeye mwenyekiti uyajadili. Nakushauri um'bembeleze mwenyekiti wako akurudishie akili zako, ili uwe huru kujadili mambo yako.
 
Alaska haijawahi kuomba kuwa sehemu ya Marekani, Alaska ilinunuliwa na Marekani na iliuzwa na Russia
Sawa mkuu, na hawa wangeenda mezani mpunga ukalipwa nchi ikawa chini ya wababe wa dunia, na wananchi wakaanza kuishi maisha ya New York, Calfornia, Chicago nk.
 
Russia nae anaipata pata
IMG_20220225_092829.jpg
 
Mkuu mbona kuna nchi nyingi tu zimeamua kuwa chini ya himaya fulani yenye nguvu bila kujali jiografia au umbali uliyopo ili kulinda usalama wa sehemu husika. Mfano wa Franch Guiana hii ipo Amerika ya kusini ikipeana mpaka na nchi za Amerika ya kusini kama vile Brazil nk. Kisiwa hiki kimeamua kuwa chini ya himaya wa wafaransa na mpaka leo inatambulika kuwa ni moja kati ya sehemu iliyo chini ya mamlaka ya ufaransa. Kwahiyo hata hawa wa Ukraine wangeyafanya haya zamani, upuuzi huu wa leo usingejitokeza.
Huko umempeleka mbali sana; mrudishe hapa Mayotte ambao wako chini ya Ufaransa
 
Sema Urusi amechukua maamuzi ya haraka sana bila kuangalia madhara ya baadae, killing of innocent people is totally unacceptable, mimi nahisi Putin amenunua silaha nyingi sana na alikua anatafuta pa kuzitimia maana ameona zinakaa tu hazina kazi sasa anata kuonyesha ulimwengu kwamba ana stock ya kutosha

Natamani wasitishe hii vita maana raia na watu wasio na hatia wanateseka, shughuli za maendeleao zimekwama, uchumi utatikisika na mbaya zaidi wanazalisha wakimbizi ilhali funia bado ipo kwenye janga la Korona
 
Alichofanya Putin kitaigharimu nchi yake miaka mingi ijayo. Hii chance ilikuwa inatafutwa na nchi za magharibi (hasa Marekani) muda mrefu sana ili waweze kupata mwanya wa kuingiza silaha zao na mamluki wa magharibi mpakani mwa Urusi. Kwa vile nchi iko katika vita ni ngumu ku control silaha zinazoingizwa, na mamluki wa magharibi ambao wengine wana asili ya Ukraine wanaoingia kutoka upande wa Poland, Georgia nk. Hii inamaana hata vita itaposimama tayari mmarekani na washirika wake watakuwa washafanikiwa kuweka silaha zake na mamluki wake (jeshi) katika mipaka yote ya Ukraine na Urusi. Sasa hapo ndio hali itapokuwa mbaya zaidi kwa usalama wa Urusi kupitia mipakani kwake. Lets wait to see.
 
Kwahiyo unataka kusema hamna mamlaka wa Russia nchini Amerika. Vita ishaisha hiyoo, na ujumbe umewafikia wanafki wote wa Dunia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo unataka kusema hamna mamlaka wa Russia nchini Amerika. Vita ishaisha hiyoo, na ujumbe umewafikia wanafki wote wa Dunia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mamluki wanaweza kuwepo lkn wasiwe na uwezo kivile, yani uwezo wa kupindua meza au mipango iliyowekwa na Marekani.
 
According to reports in response to yesterdays sanctions in the UK, Russia has reportedly closed its airspace to all UK affiliated aircraft.
 
Back
Top Bottom