Kwanini Ukraine haikuomba kuwa sehemu ya USA ili kuepusha huu ujinga unaoendelea sasa?

Kwanini Ukraine haikuomba kuwa sehemu ya USA ili kuepusha huu ujinga unaoendelea sasa?

Mkuu mbona kuna nchi nyingi tu zimeamua kuwa chini ya himaya fulani yenye nguvu bila kujali jiografia au umbali uliyopo ili kulinda usalama wa sehemu husika. Mfano wa Franch Guiana hii ipo Amerika ya kusini ikipeana mpaka na nchi za Amerika ya kusini kama vile Brazil nk. Kisiwa hiki kimeamua kuwa chini ya himaya ya wafaransa na mpaka leo inatambulika kuwa ni moja kati ya sehemu iliyo chini ya mamlaka ya ufaransa. Kwahiyo hata hawa wa Ukraine wangeyafanya haya zamani, upuuzi huu wa leo usingejitokeza.
Huko mbali : kuna French Mayotte iko Africa lakini iliamua kuwa sehemu ya Ufaransa
 
They are clearly already prepared for any sanction they could face, they wouldn't have invaded if sanctions would bring them down
 
European benchmark nat gas TTF falls ~20% early on Friday as Russian gas flows into the EU (via Ukraine) surge. European utilities are asking Gazprom to ship more gas, and the Russian state-owned giant is happy to oblige. Capitalism in times of war | #Ukraine #UkraineInvasion
 
Huko mbali : kuna French Mayotte iko Africa lakini iliamua kuwa sehemu ya Ufaransa
Asante kwa kunikumbusha na hili mkuu. Ukweli ni kwamb Russia imeweza kuivamia Ukraine kwa sababu nchi hiyo sio sehemu ya ardhi ya Marekani, na wala ilikuwa bado haijajiunga rasmi na Nato. So wakubwa wa Dunia wakiongozwa na USA hawana maslahi nayo nchi hiyo ya moja kwa moja ambayo yangewashawishi kuingia na wao vitani. Kama mrusi kweli anampango wa kurudisha juhudi za Nato nyuma, basi angeanza kwanza kuvamia hizo nchi nyingine za jirani yake ambazo tayari zimeshajiunga na Nato muda mrefu, zina silaha na wanajeshi wengi wa Nato katika ardhi zao ambazo zinapeana mpaka na Russia. Kuivamia nchi ambayo bado haijawa mwanachama rasmi wa Nato, na kuziacha zile ambazo ni wanachama halisi wa Nato, ni dalili ya mkwara na uonevu dhidi ya nchi isiyokuwa na uwezo wa kujitetea ambayo sheria za Nato haziruhusu wao kumpigania kwa vile sio mwanachama wao na pia nchi yenyewe bado hawajawa na maslahi nayo kivile. Hapo pichani ni nchi zilizojiunga na Nato miaka mingi iliyopita. Nchi hizi ni jirani kabisa na Russia lkn kamwe Russia haijafikiria au kuota kuzivamia, kwani anajua kitachotokea kwake endapo atathubutu kufanya hivyo kwa moja ya nchi iliyo chini ya Muungano wa Nato.

images.jpeg
 
Sema Urusi amechukua maamuzi ya haraka sana bila kuangalia madhara ya baadae, killing of innocent people is totally unacceptable, mimi nahisi Putin amenunua silaha nyingi sana na alikua anatafuta pa kuzitimia maana ameona zinakaa tu hazina kazi sasa anata kuonyesha ulimwengu kwamba ana stock ya kutosha

Natamani wasitishe hii vita maana raia na watu wasio na hatia wanateseka, shughuli za maendeleao zimekwama, uchumi utatikisika na mbaya zaidi wanazalisha wakimbizi ilhali funia bado ipo kwenye janga la Korona
Ni kweli mkuu, kama Urusi ina lundo la silaha ni bora wangekuja kuipa Kongo ipambane na waasi wake huko maporini, kuliko kuzitumia kwa watu wasiokuwa na hatia yoyote.
 
embu chukua atlas uangalie vizuri ramani ya dunia halafu labda kuna kitu utagundua. Ni sawa na useme kigamboni iwe sehemu ya mkoa wa kigoma badala ya dar es salam.
Hoja yako haina nguvu mkuu. Ukraine ni nchi huru ambayo inaweza kujiamulia chochote bila kuingiliwa na Taifa lolote la nje, Kigamboni ambayo ipo katika mkoa wa Dar es salaam, na Kigoma vyote vipo chini ya mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo ndio tofauti yao.
 
Kutokana na ukaribu wa ki mipaka, baina ya ukraine na urusi, ni ngumu sana kwa Urusi kukubali hilo litokee, kwani poland ilipoingizwa NATO, urusi sasa anaona huko kunakoelekea siko, ndio wakawa wamekubaliana kuwa NATO, asizidi kujipanua kuelekea mashariki!!

Na putin hataki kuiona ukraine ina ingia NATO, ila ukraine hata kwenye katiba yao tayari waliisha weka, road map ya kujiunga NATO!!Kwani ndio wanaona itakuwa salama yao!!

Ila putin sasa anataka kuweka uongozi mpya hapo ili aweze kuu control, kama anavyofanya kwenye nchi nyingi za iliyokuwa USSR.
NATO-MNATO
 
Back
Top Bottom