Kwanini Ukraine haikuomba kuwa sehemu ya USA ili kuepusha huu ujinga unaoendelea sasa?

Huko mbali : kuna French Mayotte iko Africa lakini iliamua kuwa sehemu ya Ufaransa
 
They are clearly already prepared for any sanction they could face, they wouldn't have invaded if sanctions would bring them down
 
European benchmark nat gas TTF falls ~20% early on Friday as Russian gas flows into the EU (via Ukraine) surge. European utilities are asking Gazprom to ship more gas, and the Russian state-owned giant is happy to oblige. Capitalism in times of war | #Ukraine #UkraineInvasion
 
Huko mbali : kuna French Mayotte iko Africa lakini iliamua kuwa sehemu ya Ufaransa
Asante kwa kunikumbusha na hili mkuu. Ukweli ni kwamb Russia imeweza kuivamia Ukraine kwa sababu nchi hiyo sio sehemu ya ardhi ya Marekani, na wala ilikuwa bado haijajiunga rasmi na Nato. So wakubwa wa Dunia wakiongozwa na USA hawana maslahi nayo nchi hiyo ya moja kwa moja ambayo yangewashawishi kuingia na wao vitani. Kama mrusi kweli anampango wa kurudisha juhudi za Nato nyuma, basi angeanza kwanza kuvamia hizo nchi nyingine za jirani yake ambazo tayari zimeshajiunga na Nato muda mrefu, zina silaha na wanajeshi wengi wa Nato katika ardhi zao ambazo zinapeana mpaka na Russia. Kuivamia nchi ambayo bado haijawa mwanachama rasmi wa Nato, na kuziacha zile ambazo ni wanachama halisi wa Nato, ni dalili ya mkwara na uonevu dhidi ya nchi isiyokuwa na uwezo wa kujitetea ambayo sheria za Nato haziruhusu wao kumpigania kwa vile sio mwanachama wao na pia nchi yenyewe bado hawajawa na maslahi nayo kivile. Hapo pichani ni nchi zilizojiunga na Nato miaka mingi iliyopita. Nchi hizi ni jirani kabisa na Russia lkn kamwe Russia haijafikiria au kuota kuzivamia, kwani anajua kitachotokea kwake endapo atathubutu kufanya hivyo kwa moja ya nchi iliyo chini ya Muungano wa Nato.

 
Ni kweli mkuu, kama Urusi ina lundo la silaha ni bora wangekuja kuipa Kongo ipambane na waasi wake huko maporini, kuliko kuzitumia kwa watu wasiokuwa na hatia yoyote.
 
embu chukua atlas uangalie vizuri ramani ya dunia halafu labda kuna kitu utagundua. Ni sawa na useme kigamboni iwe sehemu ya mkoa wa kigoma badala ya dar es salam.
Hoja yako haina nguvu mkuu. Ukraine ni nchi huru ambayo inaweza kujiamulia chochote bila kuingiliwa na Taifa lolote la nje, Kigamboni ambayo ipo katika mkoa wa Dar es salaam, na Kigoma vyote vipo chini ya mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo ndio tofauti yao.
 
NATO-MNATO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…