Kwanini Ukristo na Uislam unashamiri kwenye nchi masikini na duni kielimu?

Kwanini Ukristo na Uislam unashamiri kwenye nchi masikini na duni kielimu?

Si unaona sasa watanzania vile akili zenu mbovu. Na hii si kashfa bali ni ukweli.
Wewe mtu anatoa hoja ingine wewe unaikwepesha na kujenga ya kwako ili ulete fitna ya udini humu!.
Hivi nyie watu mtaendelea lini na kuwa na fikra wazi. Halafu unapochangia hoja wacha ujinga wa kutuandikia maneno mawili matatu ya kiingereza ili tukuone umesoma. Huo ni utumwa wa kiakili. Watu wanfahamu hicho kiingereza bora kuliko wewe lkn hapa sio mahala pake. Hii inatwa JAMII FORUM na sio society forum.
 
Kwanza kabisa Mkuu tambua nini maana ya zakah

Zakah ni kodi inayolipiwa mali ya Muislamu ili wapewe maskini lengo ni kujiendelza kiuchumi ili mwaka unaofuta na wao waweze kulipa zakah watakayopewa maskini wengine ili wajiendeleze kuichumi.Mtu akishapewa Zakah anatakiwa afiatiliwe anaifanyia nini hiyo zakah pia apewe elimu ya matumizi wa hiyo zaka,sio kwenda kwenda kununua kuku na mchele ufaidi siku moja ili keshoukachukue zakah nyingine.

Ama Sadaka anapewa mtu yoyote yule maskini au tajiri(maskini anastahiki zaidi kuliko tajiri),sadaka anatoa mtu yoyote yule.

Hao matajiri wanaowapangisha watu foleni misikitini wanawadhalilisha maskini tu,hawataki kulipa zakah

Allah Mtukufu amesema katika Qurani Tukufu"Allah ameharamisha Riba na Amehalalisha Biashara"
Akasema tena"Akika ya Allah anaipa baraka mali ya biashara na inaipungizia baraka mali ya Riba"
Akasema tena"Anayekula Riba ametangaza vita na Allah"

Katika uislamu Riba ni haramu hata uipake rangi gani.

Riba sio haramu ni jinsi gani tu inavyoitwa kulingana na imani husika. Cha msingi ni kwamba mikopo yote ina rudishio fulani, sasa hapa tunapata kiuhalisi athari nyingine ambazo dini zinavyotudhulumu kiakili (brainwash) kutusadikisha/kutudanganya/kugeuzageuza maneno n.k
 
nani anaweza kueleza maana halisi ya dini? unajua inabidi mtu uende mbali sana ili ujue kwa nini hao wenye ngozi nyeupe walitumia dini ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutunyonya na sasa wanaona hazina maana tena. Elewa kuwa dini na siasa zinatumika kutawala fikra za binadamu. ukitaka kuelewa zaidi tafuta kitabu cha mwanafalsafa SPINOZA
 
Please, Thread hii sikuileta kwa ajiri ya kudodosa uharali na uzuri wa dini fulani against dini nyingine. Kwa wale watu wenye fikra finyu hapa ambao wanafikiria dini yao ni bora kuliko dini nyingine, HII SIYO THREAD ILIYOLETWA KWA AJIRI YA MARUMBANO HAYO. Sihitaji hiyo michango kwenye THREAD HII.

MOD's kwa busara na uelewa wao, ndiyo maana wakaiweka kwenye jukwaa la siasa kujibu maswali kama yalivyobainishwa na tafiti mbali mbali kuhusiana na uhusiano wa umaskini na elimu duni kufungamana na dini za kikristo na kiislamu.
 
nani anaweza kueleza maana halisi ya dini? unajua inabidi mtu uende mbali sana ili ujue kwa nini hao wenye ngozi nyeupe walitumia dini ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutunyonya na sasa wanaona hazina maana tena. Elewa kuwa dini na siasa zinatumika kutawala fikra za binadamu. ukitaka kuelewa zaidi tafuta kitabu cha mwanafalsafa SPINOZA
Mkuu Mangio ,
Kwanza kama ninavyofahamu neno DINI linatokana na lugha ya kiarabu Din kama kiswahili kilivyopatikana. Hili ni neno pana na maana yake hata imeelezwa pia tofauti tofauti na wana socialogy, pschologist and naturalist

Kwa ujumla, dini ni mfumo wa maisha ambao watu wamejichagulia na kuufuata katika maisha yao. Huu mfumo umejengeka katika nguzo kuu mbili ambazo ni Imani (ibada) na Desturi.

Imani ni mtindo wa maisha unaowafanya watu kuwa wamoja katika mitazamo na mambo ya kiroho. Hapa ndipo jamii inapobainisha lipi ni ovu na lipi siyo ovu katika matendo yao kwa kuogopa nguvu ambayo inawafanya waamini kama ni kubwa zaidi ya uwezo walionao. Lakini katika kufanya hivi, hujikuta kunazaliwa mifumo tofauti ya kidini ambayo pia huzaa madhehebu tofauti.

Desturi katika dini huzaa matendo na taratibu katika maisha yetu ambapo ndiyo unakuta matendo katik mifumo ya kipagani, kishirikina, kikomunisti, kibepari, kijamaa na kadhaiika.

Watu wengi huwa wana jikita kwenye sehemu moja tu ya maana ya dini ambayo ni imani wanasahau kuwa katika dini lazima kuwepo na desturi iliyobumiwa na mwanadamu katika maisha kwa ajiri ya jamii fulani (Desturi binadamu).
 
Last edited by a moderator:
Ng'wamapalala, Wewe hauelewi Ukirsto hata kidogo, Kama unadhani ukirsto ni madhebu umeliwa, The great success of USA and UK is Biblical, I mean umesababishwa na Nguvu zinazoaminiwa na Wakiristo, sasa unaposema ukirsto ni rafiki wa umasikini sikuelewi.
 
Dini zipo associated sana na moral development. Katika nchi zilizoendelea, watu wana maadili hata kama hawapractice dini. Rushwa, uzinzi, dhulma, uongo, wizi na mengine yanaitwa maovu katika jamii zilizoendelea lakini yanaitwa dhambi katika nchi zisizoendelea. Pengine hii inahusishwa pia na degree ya ustaarabu, ambapo mara nyingi ni kubwa katika jamii zilizo na elimu kuliko jamii ambazo hazijaelimika

Labda tuchukulie katika Tanzania mikoa ambayo ina wasomi wengi kama Mwanza, Shinyanga huku wanaongoza kwa kunyofoa viungo va albino. Mbeya huku wanaongoza kwa kuchuna ngozi, Moshi na Arusha biashara ya vilevi na ujambazi.

mambo ambayo katika mikoa duni kielimu kama Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga hayapo.

Labda utudadavulie neno ustaharabu umemaanisha nini?.

Ng'wamapalala, Wewe hauelewi Ukirsto hata kidogo, Kama unadhani ukirsto ni madhebu umeliwa,
Mkuu Sangarara sijasema Ukiristo ni madhehebu ila ninachosema hakuna mkiristo duniani asiye na dhehebu. kwa maana kuwa, huwezi kulitenganisha dhehebu na Ukristo.
The great success of USA and UK is Biblical, I mean umesababishwa na Nguvu zinazoaminiwa na Wakiristo, sasa unaposema ukirsto ni rafiki wa umasikini sikuelewi.
Ninafikiri unashindwa kuielewa vizuri point nilikuwa nimetengeneza. Kwa kifupi tu ni kwamba, Ukristo na Uislam huwa unakufa pale jamii inapokuwa tajiri kielimu na kimaslahi. Historia ya UK inajulikana kabisa kwa jinsi nchi hii ilivyotumia dini kama kiingilio cha utawala wa kikoloni katika nchi mbali mbali hapa duniani. Na katika ukoloni huu, nchi hii ilitajilika kutokana na kuzoa malighafi katika nchi koloni zake.

Watu waliosombwa na kupelekwa USA kufanya kazi katika mashamba na viwanda walitumia dini kama kujifariji ama njia ya kuponya psychologically majeraha ya kazi ngumu za kila siku kwa kuamini kama Mungu yupo na kuna siku moja kila kitu kitakuwa kama wanavyoamini. Katika kusubiri siku hiyo, ndiyo kila siku waliendelea kufanya kazi ngumu na nzito kuwatajirisha mabwenyeye huku wao wakiendelea kuwa maskini.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Sangarara sijasema Ukiristo ni madhehebu ila ninachosema hakuna mkiristo duniani asiye na dhehebu. kwa maana kuwa, huwezi kulitenganisha dhehebu na Ukristo.

Ninafikiri unashindwa kuielewa vizuri point nilikuwa nimetengeneza. Kwa kifupi tu ni kwamba, Ukristo na Uislam huwa unakufa pale jamii inapokuwa tajiri kielimu na kimaslahi. Historia ya UK inajulikana kabisa kwa jinsi nchi hii ilivyotumia dini kama kiingilio cha utawala wa kikoloni katika nchi mbali mbali hapa duniani. Na katika ukoloni huu, nchi hii ilitajilika kutokana na kuzoa malighafi katika nchi koloni zake.

Watu waliosombwa na kupelekwa USA kufanya kazi katika mashamba na viwanda walitumia dini kama kujifariji ama njia ya kuponya psychologically majeraha ya kazi ngumu za kila siku kwa kuamini kama Mungu yupo na kuna siku moja kila kitu kitakuwa kama wanavyoamini. Katika kusubiri siku hiyo, ndiyo kila siku waliendelea kufanya kazi ngumu na nzito kuwatajirisha mabwenyeye huku wao wakiendelea kuwa maskini.

Ng'wamapalala
Kwa hiyo wewe unaamini kwamba wale jamaa waliokuja kwa gia ya ukirsto kuleta ukoroni na uny'ang'anyi chungu nzima Africa walikuwa ni wakirsto (kama ukirsto unavyoelezewa kwenye biblia) au walikuwa ni matepeli tu?

Sidhani kama ni sahihi kuchukulia mambo juu juu, wakati Ukirsto umeandikwa kwa ufasaha kabisa kwenye Biblia, point yake ni kwamba jinsi unavyorelate mambo haya na Ukiristo si sahihi kwa sababu hayako supported na biblia, au la Biblia sio the right reference kuelezea ukirsto.
 
Back
Top Bottom