Kama wewe ni muumini mmojawapo wa dini hizi mbili utaelewa ninachokisema hasa kama hupendi kuidanganya nafsi yako. Tangu malalamiko ya wananchi, mashirika na wadau mbalimbali kuwa kuna ombwe la uongozi tangu jk aingie ikulu waumini wa dini hizi mbili walianza kuumana hadharani kwa maneno; kwanza kama utani kisha kama vita vya maneno.
Wale waliobahatika kuhudhuria mihadhara ya malumbano ya kidini wataniunga mkono kwa sababu ilikuwa inatia hamasa kupinga kauli ya upande mmoja tena mbaya zaidi kwa kutumia misahafu ya dini husika. Siku moja nilihudhuria kwa dakika chache ikanilazimu kushindwa kuvumilia kusikiliza maneno yaliyokuwa yakitolewa kukashifu dini fulani kuwa wanaruhusiwa kuwafira/kuwalawiti wake zao! Kumbuka hapa ni kupeana vidonge kwa zamu kulingana na muda mliopangiana. Serikali ilikuwepo na polisi walihusika kutoa vibali! Jamani hivi tumlaumu nani kwa kutuchonganisha kama siyo rais wetu?
Mwaka 2004/2005 kulitokea sintofahamu kati ya wakristo na waislam baada ya waislam kuendesha mhadhara wa kukashifu ukristo, kisha wakristo kuendesha mhadhara kama huo wiki iliyofuata huku wakikashfu taratibu za hitma/arobaini ya waislam kiasi kwamba wakristo wakaanza kuingia tashwishwi kushirikiana na waislam katika masuala ya vyakula ikiwemo kuchinja.
Mzunguko wa mihadhara hiyo nchi nzima kuliwazindua watu (negatively or positively) kuhusu ushabiki na chuki za kidini. Tangu hapo watanzania wengi tumeingizwa kwenye mtego huo hasa wanazi wa ukristo na uislam! Tunapokataa uwepo wa udini kama kinamwigulu nchemba tunaharibu kabisa maana badala ya kutibu tunabomoa. Nafsi zetu zinajua tulivyo! Hata rais kikwete anaijua nafsi yake juu ya suala hili! Wakristo na Waislam wa kweli wanalijua hili na wanatamani suluhu ipatikane.