Kwanini Ukristo na Uislam unashamiri kwenye nchi masikini na duni kielimu?

Kwanini Ukristo na Uislam unashamiri kwenye nchi masikini na duni kielimu?

Ng'wamapalala,,
Thanks kwa mada yako njema mkuu,

Lakini kwa maono yangu mimi ni kwamba zipo nchi ambazo zimeamua kuuchukua mfumo wa kisecular kama ndio suluhisho kuu na msingi mkuu wa maisha yao na kuzifanya dini kama fashion tu, au kitu cha kutumika kwenye matukio kama ya misiba, sherehe za ndo na n,k.,
Mkuu THE BIG SHOW , ninakubaliana na wewe, lakini nyingi ya nchi hizo ambazo ni tajiri na wananchi wenye viwango vya elimu ya juu, kihistoria wananchi wake walikuwa wanaishi ndani ya imani ya hizi dini, lakini kadri walivyokuwa wanaelimika na kutajirika, ndivyo pia walivyokuwa wanaachana na imani za dini hizi mbili.
Pia sijafaham vyema hapo kuhusu nchi hizo maskin umeangalia kitu gani hasa, zipo nchi kama Iran, Qatar, Saudi Arabia etc ambazo si maskini kwa kias hicho, kwa ufupi ni watu wenye per capital icomes kubwa lakini wana iman zao thabiti tu za kikristo na kiislam. Thanks..
Nimejaribu kuangalia nchi ambazo hazina utajiri mkubwa wa kuridhi kama mafuta kubainisha tofauti na correlation ya umasikini na elimu duni kwa nchi zenye neema ya hizi dini mbili. Kumbuka pia, hiyo ni idadi ya nchi ambazo zimehusishwa katika research na zimenifanya kupata bainisho hili.
 
Last edited by a moderator:
mkuu naomba nijibu bila kutafuta angalizo, yaani nitoe maana kwa mazingira.
Riba ni rejesho la ziada kwenye Amana, yaani ni ziada ya mali/dhamani ya kitu ulichopewa na mtu/tasisi.
hii inafidia mtu kuacha kutumia amana yake leo akaukupa wewe nguvukazi mikono utumie leo halafu mrudishie siku za mbeleni.
kwanini nimeihusisha na ijir, murakhabar etc, kwenye mfumo wa benki za kislam, mfanya biashara aliyekopa akipata faida tunagawana( benk na mteja) hivyo benki inapata fedha zilizokopwa jumlisha faida ya hiyo biashara ya mteja!!! kwa kifupi inapata principle plus share of profit!!!
Traditional banks, haziangalii faida, ila zinategemea utapata faida na utalipa kiasi ulicho kopa jumlisha ziada ( toka kwenye faida ya bishara/shughuli yako)
wewe unajua je mkuu? nipe darasa
SP

Mkuu unajua tofauti baina ya Riba na Biashara?
 
Mkuu THE BIG SHOW , ninakubaliana na wewe, lakini nyingi ya nchi hizo ambazo ni tajiri na wananchi wenye viwango vya elimu ya juu, kihistoria wananchi wake walikuwa wanaishi ndani ya imani ya hizi dini, lakini kadri walivyokuwa wanaelimika na kutajirika, ndivyo pia walivyokuwa wanaachana na imani za dini hizi mbili.

Nimejaribu kuangalia nchi ambazo hazina utajiri mkubwa wa kuridhi kama mafuta kubainisha tofauti na correlation ya umasikini na elimu duni kwa nchi zenye neema ya hizi dini mbili. Kumbuka pia, hiyo ni idadi ya nchi ambazo zimehusishwa katika research na zimenifanya kupata bainisho hili.

Tanzania mbona tuna utjiri mkubwa wa kurithi wa rasilimali kebekebe,mbona bado ni maskini wa kutupwa.

Acha kusingizia Dini ni watu wenyewe akili zetu za kushikiwa
 
Umetumwa kuleta Dini za Kutembea Uchi barabarani,Ukahaba na Ushoga ili uendelee kupata ufadhili huko magharibi,haya ujumbe umefika nenda kachukue posho yako kwa mabwana zako mashoga na wasagaji ndio maendeleo yanu hayo
Mkuu kunijadili mimi ni kupoteza muda wako ambao ninatumaini ni aghari. Jadili kilichoko chakula kilichoko mezani na siyo mpishi.

Kutaka kuuficha au kutousikia ukweli hakuondoi ukweli. Ukweli utabakia kuwa ukweli hata kama utaukimbia.

Hili ni jukwaa la kupashana habari, kuelimishana na kukosoa hoja na siyo mtu.

Mkuu kosoa hoja kwa kujenga hoja, siyo kupiga kelele huku umeficha hoja yako.
 
Wakati wa kipindi cha giza huko Ulaya Wajanja wachache Ulaya walitumia Dini kwa maslahi yao binafsi,watu wa Ulaya wakapigwa changa la macho na viongozi wa Dini,tatizo halikuwa Dini bali tatizo lilikuwa viongozi wa Dini.

Sasa baada ya kupigwa changa la macho kwa kunyonya na kudumazwa akili na viongozi wa Dini sasa hivi westren Countries wameanzisha Dini yao ya matamanio ya nafsi kwa kutembea uchi,ukahaba,ushaga na usagaji na wanawalaizimiaha wengine wafuate hiyo Dini yao ndio wamemtuma huyu mleta mada hapa
 
Wadau,
Umaskini una uhusiano wa karibu na ugawanaji wa mali. Kwenye nchi zenye umaskini amabzo mara nyingi ugawanaji wa mapato hauko sawa njia pekee ya kutajirika ni kuingia kwenye uongozi hasa pale unapokuwa na uwezo wa kucontrol kipato kinachopatikana kwa njia ya kodi au nyingine. Hii ndiyo sababu mojawapo ya dini kushamiri katika nchi hizi kwa sababu kuna viongozi wa dini ambao wanacontrol sadaka/zaka na wanaipenda kazi yao ndiyo sababu kila mmoja anajitahidi kupata waumini wengi ili aweze kupata mapato mengi. Kwangu mimi sadaka, zaka na kodi naona vyote sawa tu

Jingine inawezekana kushamiri kwa dini kunakuja baada ya umaskini kuzidi kwenye jamii. Watu inawalizimu wakubali kushindwa katika maisha haya na wanaweka matumaini yao ya kuishi maisha bora katika maisha yajao (baada ya kufa) ambayo hatujui kama yapo au hayapo.

Serikali ingeweka masharti kila jengo la ibada liwe na shule (ilim duniya) pamoja na hospitali kwa ajili ya kusaidia jamii
 
napata mashaka na huu utafiti! vigezo gani vilivyotumika kuthibitisha dini inaleta umasikini?kwa maana umeweka nchi zenye mazingira tofauti ya kidini,kuna nchi humo ni za kiislamu tu,kuna zingine ni za kikristo wakati zingine ni mchanganyiko wa ukristo na uislamu

katika zote hizo sababu za kuwa masikini zinatofautiana labda unijuze zaidi mana research inaonekana too general Ng'wamapalala
 
Ng'wamapalala,

Asante sana kwa kunialika katika mjadala huu mzuri; kwa kweli nikiri kwamba mimi sina utaalamu wala uzoefu wowote wa maana katika suala husika, kwahiyo nitachofanya hapa ni kutoa tu mawazo yangu na ninasimama kupingwa:

Kwanza nakubaliana na hoja kwamba economic performance ya jamii fulani has something to do with dini lakini nakataa pia kwamba such a performance is a function of a certain religious doctrine; Nitajaribu kufafanua:

Nadhani wengi wetu tunakubaliana kwamba kilichonyanyua uchumi wa jamii mbalimbali duniani - jamii mbalimbali za magharibi, mashariki ya kati, afrika n.k na hata kabla ya ukoloni was TRADE; Kwa maana nyingine, Trade is what sparked economic growth, development, hivyo military strengths katika jamii mbalimbali; sasa kilichokuja tofautisha mafanikio ya jamii moja dhidi ya nyingine ikaja kuwa ni matumizi ya such strengths kutaka ku dominate wengine ili uwe na surplus kutokana na pressure mbalimbali za ndani ya jamii husika;

Kama tupo pamoja so far, tukirejea katika historia ya dunia kwa ujumla, both wakristo, waislamu, wahindi, budhists na hata waumini mizimu katika jamii zetu afrika wakati ule kama wahehe, wahaya, wakamba, wanyamwezi n.k, wote hawa walifaidika sana na TRADE na ikawa ni kichocheo kikubwa sana cha economic growth, scientific development, na ustawi wa jamii zao kwa ujumla; upo ushahidi tosha kwamba baadhi ya inventions katika nchi tajiri za leo zilitokana na traders wa nchi hizo kuiba ideas, tools from africa, asia n.k kisha kwenda kuzifanyia more improvements na baadae sasa walipokuja to conquer these societies, wakawaingiza katika mfumo wa to produce what they didn't consume and consume what they didn't produce, tatizo ambalo ni mataifa machache sana ambayo yameweza kulitatua katika karne iliyopita yani 1900 - 2000;

Kwa maana hii, mtazamo wangu ni kwamba mafanikio ya kiuchumi don't depend on one particular religious doctrine but other exogenous factors kama nilivyojadili hapo juu; ndio maana karne ya 20 na sasa 21 zitaendelea kutawaliwa na clashes of civilization kwani dini moja ndio imejiona kwamba ina mamlaka to set the world order na sio out of consensus bali kupitia military mighty;

Nimalizie kwa kusema kwama - economic performance is an outcome ya culture ya mtu au jamii yake, and as we know, culture ni moja ya key dimensions of religion; And culture influences economic outcomes in a major way kwani it affects personal traits kama honesty, nidhamu katika matumizi ya fedha (kuepuka ubadhirifu), willingness to work hard, openness to strangers (ambayo ni muhimu for business or commercial success) n.k; kwa maana hii, mkinga, mpemba, mchaga, myoruba, mzulu, mwingereza, mchina, mhindi, mjapani n.kn wote wana religious beliefs and practices that are needed to succeed in commercial ventures based on budhism, hinduism, islam, christianity and how these religions or cultures influences economic outcomes per my discussion above;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, Utafiti haukufanyika katika nchi hizi kwa sababu utajiri mkubwa iliyonao ni wa kuridhi (mafuta) na siyo wa kutengeneza siku baada ya siku.

Mkuu katika hizo nchi ulizotaja tajiri na zisizokuwa na dini, ni nchi gani haina utajiri wa asili (kurithi)?

Ninachoamini ni kuwa waafrika tulichelewa kuamka na wazungu wakaja kupora utajiri wetu wa asili na kuchangia sehemu ya umaskini wetu.

Hata hivyo, umasikini wa nchi kama Tanzania, hautokani na dini ila ni ujinga wetu wenyewe.

Dini ni maumbile ya mwanadamu kwamba lazima naturally mwanadamu atakuwa affiliated na imani moja ama nyingine kutokana na maumbile ya mungu. Therefore, hata tungezaliwa kuwa matajiri, bado watu wangekuwa na dini zao.
Unaweza kutuonesha kwamba dini zetu zimechangia vipi katika umaskini tuliokuwa nao?
 
Ninavyofahamu na kuona S/Korea, China na nchi nyingi za Far East, Ukristu unakua na hii ni kwasababu religion ni natural kwa mwanadamu. Communism ilikufa kwa vile ilikuwa na vacuum.

Hizo nchi hapo juu si masikikini kihivyo,.ukristo wa korea na uchina,hongkong,macau etc upo kwa matajiri,hata west watu wanaorudi ktk ukristu wapo.

North Korea na China wanaangalia ukristu kama tishio kwa tawala za kijamaa kuliko chombo cha mafanikio. Ingawa raia wake wana-fight kuufuata wakiamimini ndio ustaarabu wa mafanikio.

Ukristu korea si majority religion ila impact yake dunia inaona na hata wamisionary wao ni wengi sana dunian.

Tuwe waangalifu, East panakuwa huku wakipokea ukristu, west panaanguka jinsi wanaukataa ukristu. Jamii isiyo na hope ni kama mfu. Yesu ni hope.

Atheism haimpi mtu sababu ya kujenga kitu cha kudumu. Islam inakimbiza watu wafe kuwahi pepo zaidi kuwekeza ktk elimu dunia .
Tuwe waangalifu na tafiti za propaganda km za redet. Hata mashoga wana tafiti zao kuonyesha kuwa hata penguin mashoga wapo,nyani mashoga wapo na wanyama wengine halafu wakahitimisha kuwa ni natural. Lakini nani kawauliza waliwapataje hao wanyama wachache mashoga? Kama si wao waliwaprogram ili potosha dunia.

cc Kiranga

1. Kitu kuonekana "natural" sio maana yake kwamba muonekano huo "natural" ni actual. Ukiweka maji yajae robo tatu ya glasi, halafu uweke penseli vertically cross sectional na kuiangalia kutoka nje ya glasi utaona penseli imepinda, wakati kiukweli haijapinda (refer to light rays and refraction in different media). Kwa hiyo kusema "this seems natural" is the first step towards accepting wrong conclusions and non-sequiturs.

To natural sight, the natural conclusion is that the earth is flat. That does not make the earth flat. We ought to be careful enough to not simplify complex issues and not make unnecessarily complex the simple issues.

2. Your argument is narrow and shorchanging the subject because it is comparing Communism and Christianity instead of examining broader issues. Why pick and choose pockets of defeated communism that shows Christianity as rising and not look at the Scandinavian countries (high economic achievements, high education) where Christianity is being rejected?

3. Hope is neither good nor bad. Matumizi yake ndo yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Mtawala anayetaka kuwafunga watu wake katika umasikini anaweza kutumia hope kuwazubaisha, kwamba maendeleo yapo just around the corner. Hapa huwezi kusema jamii isiyo na hope ni kama mfu, hapa utasema jamii iliyo na hope katika situation hii hopeless ni kama mfu. Ni smallmindedness tu inayoweza kukufanya utegemee hope wakati una nafasi ya ku experiment na ku find things out. Hii ndiyo tofauti ya sayansi na dini. Kwa nini u hope wakati unaweza ku find out?

4. Kwa nini unasema atheism haimpi mtu sababu ya kujenga kitu cha kudumu? Waarabu walivyogundua kwamba jangwa lao lina mafuta viongozi wao walipata tabu sana kuwashawishi viongozi wa dini kuhusu umuhimu wa kuchimba mafuta na kutumia economic advantage hii. Viongozi wa dini walipinga kwa sababu walisema "kama allah angetaka tuchimbe mafuta angeteremsha sura kwenye Kuran kutuonyesha hilo". Sasa hapa unaweza kuona walioamini mungu ndio waliokataa kujenga mfumo wa visima vya mafuta.

Atheism inamwambia mwanadamu kwamba "hakuna mungu, do not pray to an absent god that the earth should get cleaner and pollution should be lower, do what you can to achieve these goals, live cleaner".

Sasa kati ya mtu anayejua kwamba kuomba hakusaidii (other than the therapeutic placebo effect) na kama anataka kitu akifanyie kazi yeye mwenyewe na mwingine ambaye anaendelea kukata miti na kuchafua mazingira huku akiomba mungu amsaidie kuleta mvua, nanai anajenga kitu cha kudumu? Dini inamsaidiaje huyu anayekata miti na kuomba mungu mvua ije kuifanya dunia idumu?
 
Ukiona makanisa,misikiti na ushirikina vinaongezeka kwa kasi katika jamii fulani, ni indicator ya jamii hiyo kuwa katika umasikini mkubwa, hivyo watu wanatafuta majawabu ya matatizo yao kwa kupitia moja ya njia hizo tatu
 
Mimi kwa mtizamo wangu naona kama mleta mada ana mawazo ya kimasikini na kwa wakati huo huo anahubiri utajiri. Nasema hivyo kwa ushahidi wa kile kilichopa ndani ya mioyo ya wanajamii wengi wa mazingira na sehemu tofauti. Matajiri wakubwa wa nchi kama USA na Kanada wanashangaa ikiwa masikini wa nchi kama za Afrika wanaweza kuishika dini vizuru. Halikadhalika masikini wengi wakiwa ni kutoka bara la afrika na Asia wanashangaa na kustaajabu ikiwa watu matajiri wanaweza kweli kuishika dini kikamilifu. Yaani kila kundi linawasiwasi kwa jingine, ila suala la dini haliangalii utajiri na umasikini bali ni jawabu la mioyo iliyochaguliwa kimbele (predistened) kuamini. Ni lazima watu hao wafanye hivyo katika hali yoyote kwamba ni masikini ama tajiri, ni msomi ama hakusoma. Hata hivyo ukijaribu kuhusianisha kati ya kujitambua kielimu na ujinga katika historia ya dunia utakuta kwamba hata falsafa ya maongozi ya maumbile inatoka kwa wana dini. Hata hapo ulaya ambapo wengi kwa sasa wamekengeuka wazo la kuanzishwa kwa vyuo vikuu, viwanda na mabenki liliasisiwa na wanadini na vyuo vingi vikuu vilikuwa vikimilikiwa na wanadini. Masomo yakiwa ni theologia udaktari na baadae sheria. Ukienda katika historia ya kale zaidi utakuta chuo kikuu cha kwanza kilikua nnchini Misri na waasisi wa wazo wakiwa ni wana dini.
Point nyingine, sii kweli kwamba Afrika ni masikini kama inavyohubiriwa bali ni bara tajiri ambalo linawashughulisha magharibi kutafuta rasilimali za kuwanasua na hali mbaya ya kiuchumi inayowakabili kiasa hata cha kusahau ibada. Kile kinachoitwa uwekezaji kama ukiamua kukifuatilia kwa umakini utakuta kwa asilimia kubwa ni mikataba ya kiulaghai ya mtu anaejiita tajiri kujaribu kujinasua kutoka katika hali mbaya inayomhofisha kwa kuzikwapua rasilimali za aliyembatiza jina la masikini.
Hivyo sikubaliani na mleta hoja kuwa dini inashikwa sana nchi masikini kuliko tajiri kwani kwa jinsi ninavyofahamu afrika haina watu wengi wenye dini kama nchi za magharibi. Labda iwe anashindwa kutofautisha kati ya propaganda za wanasiasa kwa mgongo wa dini(siasa za kidini).
.
 
Inawezekana ni kweli kwamba wakereketwa wa dini (fundamentalists) wapo wengi zaidi kwenye nchi maskini kuliko tajiri. Hata hivyo, sidhani kama ni sahihi kusema kwamba dini ndiyo inayosababisha watu wawe maskini kwani dini hiyohiyo kama vile ukristo unahimiza watu kufanya kazi kwa bidii huku wakimwomba Mungu wao awabariki katika kazi hizo. Kwa hiyo, dini haijasababisha watu wawe maskini. Hata hivyo, naweza nikakubaliana kwamba inawezekana baadhi ya watu wanakimbilia dini kujinusuru na hali ya umaskini waliyonayo kwa imani kuwa mafanikio yao katika maisha hayawezi kupatikana bila kumtanguliza, which is very true anyway.
 
napata mashaka na huu utafiti! vigezo gani vilivyotumika kuthibitisha dini inaleta umasikini?kwa maana umeweka nchi zenye mazingira tofauti ya kidini,kuna nchi humo ni za kiislamu tu,kuna zingine ni za kikristo wakati zingine ni mchanganyiko wa ukristo na uislamu

katika zote hizo sababu za kuwa masikini zinatofautiana labda unijuze zaidi mana research inaonekana too general ndugu Ng'wamapalala
 
napata mashaka na huu utafiti! vigezo gani vilivyotumika kuthibitisha dini inaleta umasikini?kwa maana umeweka nchi zenye mazingira tofauti ya kidini,kuna nchi humo ni za kiislamu tu,kuna zingine ni za kikristo wakati zingine ni mchanganyiko wa ukristo na uislamu

katika zote hizo sababu za kuwa masikini zinatofautiana labda unijuze zaidi mana research inaonekana too general ndugu Ng'wamapalala

Wanasema kuwa Marekani kuna udini pia pamoja na kwamba ni nchi iliyoendelea.

Cheki hiyo chart hapo chini, Tanzania haipo mbali na Marekani kwa udini.

"The chart shows that the wealthier a country is, the less important religion is to that country.

The one exception: The United States. Why?

religion.jpg


From a study:

"The clear exception to this pattern is the United States, which is a much more religious country than its degree of prosperity would suggest. Despite its wealth, the United States is in the middle of the global pack when it comes to the importance of religion.

Indeed, on this question, the U.S. is closer to considerably less developed nations such as India, Brazil and Lebanon than to other western nations."

Why do you think this is?

Source: Why Is America So Religious? - NYTimes.com
 
Wanasema kuwa Marekani kuna udini pia pamoja na kwamba ni nchi iliyoendelea.

Cheki hiyo chart hapo chini, Tanzania haipo mbali na Marekani kwa udini.

"The chart shows that the wealthier a country is, the less important religion is to that country.

The one exception: The United States. Why?

religion.jpg


From a study:

"The clear exception to this pattern is the United States, which is a much more religious country than its degree of prosperity would suggest. Despite its wealth, the United States is in the middle of the global pack when it comes to the importance of religion.

Indeed, on this question, the U.S. is closer to considerably less developed nations such as India, Brazil and Lebanon than to other western nations."

Why do you think this is?

Source: Why Is America So Religious? - NYTimes.com

mimi nachoona it has do with the degree of inequalities between the poor and the rich!kwa nchi ambazo kuna gap kubwa kati ya the poor and the rich basi udini unatumiwa na watu masikini kama silaha yao ya mapambano against the rich, but i still do not see the relationship between poverty and religion,that religion causes poverty!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Inawezekana ni kweli kwamba wakereketwa wa dini (fundamentalists) wapo wengi zaidi kwenye nchi maskini kuliko tajiri. Hata hivyo, sidhani kama ni sahihi kusema kwamba dini ndiyo inayosababisha watu wawe maskini kwani dini hiyohiyo kama vile ukristo unahimiza watu kufanya kazi kwa bidii huku wakimwomba Mungu wao awabariki katika kazi hizo. Kwa hiyo, dini haijasababisha watu wawe maskini. Hata hivyo, naweza nikakubaliana kwamba inawezekana baadhi ya watu wanakimbilia dini kujinusuru na hali ya umaskini waliyonayo kwa imani kuwa mafanikio yao katika maisha hayawezi kupatikana bila kumtanguliza, which is very true anyway.

Ukristo unaweza kuhimiza chochote kulingana na unapochagua kusoma.

Naanza kuunganisha hoja yako, na avatar yako, na ukristo unasemaje kuhusu hoja yako na avatar yako, randomly.

Wewe unayesema ukristo unahimiza kufanya kazi mtu mwingine atakwambia Yesu alisema tuwaangalie ndege hawapandi wala hawavuni lakini mungu anawatunza.

Kwamba si muhimu kufanya kazi, bali muhimu ni kumtumaini mungu, utaniambia nini hapo? Ukristo unahimiza kufanya kazi hapo?
 
EMT Thanks for that NYT article. Hapo chini kwenye comments watu wametoa vipande vya maana sana, kuanzia na the relationship between racism/white supremacy and religion in the US, mpaka the fact that the US is not necessarily that educated, mpaka the US is a big country and more regional data is needed.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom