platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,424
- 11,320
Ninakubaliana na maelezo yako lakini bado pia hukutoa kilicho nyuma ya sababu ya dini za Kikristo na Kiislamu peke yake kushamili katika maeneo ya watu masikini na wasio na elimu ya juu ukilinganisha na imani za dini zingine?
Kwanza tuangalie: Kwani misingi ya hizi Dini kuu mbili ni ipi? Imani ni nini?
Kwa ufupi Msingi wa Hizi Dini ni kuishi kwa kufuata mafundisho yaliyojengwa juu taratibu maalum na zilizowekwa na Mungu (kwa mujibu wa mafundisho yao) i.e Kupendana, kujaliana, kushirikiana, uadilifu na kuonyana juu ya mienendo isiyofaa n.k (kwa mtazamo wao).
Na la pili ambalo ni kubwa ni kuwa na Imani, kuijenga Imani na kuishi kwa Imani. Na Imani kwa mtazamo wa Ukristo ni kuwa na matarajio juu ya mambo yajayo. Imani juu ya Maisha baada ya kifo, kwamba binadamu tunakufa hilo ni jambo linalojulikana, lakini baada ya hapo? ni Imani kwamba tukifuata misingi hiyo hapo juu tuna hakika ya kuishi baadaye.
Hapa lazima tukumbuke pia kwamba Ulaya Ukristo ulianza karne nyingi zilizopita. Huwezi kusema ustaarabu unaouona leo hauna muunganiko na Ukristo. Upo uhusiano mkubwa sana. Labda kinacholeta tofauti ni kimoja tu kwao, kwamba wanaona kwa sasa wanaweza kujenga Uadilifu, Utu, kuonyana n.k pasipo kukanyaga milango ya Kanisa!
Je Imani? kuijenga Imani na kuiishi Imani kila siku ni jambo linalohitaji muda na kujitoa (kwa mujibu wa Imani hizo).
Je Wazungu wana muda huo? wa kuamka saa 12 kwenda Kanisani, Je wana muda wa kumsikiliza Pastor au Padre?
Back to Waswahili:
Lazima tujue pia hakuna matumani nje ya mfumo wa Dini hizi mbili. Joto la Umasikini ni kubwa sana na mahali pekee ambapo tumaini linaweza kupatikana ni kuwa humo. Ndiyo maana ukuaji wa hizi Dini ni mkubwa, mahali ambapo Elimu ni Duni na umasikini upo juu ni rahisi watu kupokea mafundisho, kusikiliza na kujiunga.