Ibambasi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2007
- 9,296
- 4,697
Dini pia inatumika kama namna fulani ya kupunguza pressure za umasikini. Inatoa faraja na matumaini hata kama sio tangible, inaweka hofu fulani kwa wale wanaotaka kutenda maovu.
Kwa namna fulani zimesaidia kwa baadhi ya maeneo kupunguza vitendo vya kishenzi kama kufanya mauaji kwa Imani za kishirikina. Ukijaribu kupitia historia za makabila utaona kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa haki za Binaadamu hasa mauaji, Wanawake walinyanyaswa sana lakini ujio wa Dini angalau umepunguza hayo, na sababu moja kubwa.........Hofu ya Mungu.
Sikatai kwamba hata walio miongoni mwa Waumini kuna wenye tabia kama hizo lakini angalau wanajua si jambo linalokubalika kwa Mkuu wao kuliko wote - Mungu.
La nyongeza Dini imeziba ombwe la Uongozi hasa kwenye Umasikini. Tunajua kwa nchi masikini kama zetu mlipuko wa Kijamii kutokana na kukosa matumaini unaweza kutokea, lakini kwa mtazamo wangu Dini zimepunguza makali........Kuna matumaini fulani wameyajenga kwenye nyoyo za Watu.
Vipi kuhusu mapigano ya waislamu na wakristo mfano huko Nigeria? Au kwetu juzi tu huko Buselesele? Nadhani nadhani a yako kuwa dini hizi zimepunguza hivyo unavyoiita vitendo vya kishenzi haiko sahihi.