Kwanza kabisa Mkuu tambua nini maana ya zakah
Zakah ni kodi inayolipiwa mali ya Muislamu ili wapewe maskini lengo ni kujiendelza kiuchumi ili mwaka unaofuta na wao waweze kulipa zakah watakayopewa maskini wengine ili wajiendeleze kuichumi.Mtu akishapewa Zakah anatakiwa afiatiliwe anaifanyia nini hiyo zakah pia apewe elimu ya matumizi wa hiyo zaka,sio kwenda kwenda kununua kuku na mchele ufaidi siku moja ili keshoukachukue zakah nyingine.
Ama Sadaka anapewa mtu yoyote yule maskini au tajiri(maskini anastahiki zaidi kuliko tajiri),sadaka anatoa mtu yoyote yule.
Hao matajiri wanaowapangisha watu foleni misikitini wanawadhalilisha maskini tu,hawataki kulipa zakah
Allah Mtukufu amesema katika Qurani Tukufu"Allah ameharamisha Riba na Amehalalisha Biashara"
Akasema tena"Akika ya Allah anaipa baraka mali ya biashara na inaipungizia baraka mali ya Riba"
Akasema tena"Anayekula Riba ametangaza vita na Allah"
Katika uislamu Riba ni haramu hata uipake rangi gani.
Mkuu Mangio ,nani anaweza kueleza maana halisi ya dini? unajua inabidi mtu uende mbali sana ili ujue kwa nini hao wenye ngozi nyeupe walitumia dini ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutunyonya na sasa wanaona hazina maana tena. Elewa kuwa dini na siasa zinatumika kutawala fikra za binadamu. ukitaka kuelewa zaidi tafuta kitabu cha mwanafalsafa SPINOZA
Dini zipo associated sana na moral development. Katika nchi zilizoendelea, watu wana maadili hata kama hawapractice dini. Rushwa, uzinzi, dhulma, uongo, wizi na mengine yanaitwa maovu katika jamii zilizoendelea lakini yanaitwa dhambi katika nchi zisizoendelea. Pengine hii inahusishwa pia na degree ya ustaarabu, ambapo mara nyingi ni kubwa katika jamii zilizo na elimu kuliko jamii ambazo hazijaelimika
Mkuu Sangarara sijasema Ukiristo ni madhehebu ila ninachosema hakuna mkiristo duniani asiye na dhehebu. kwa maana kuwa, huwezi kulitenganisha dhehebu na Ukristo.Ng'wamapalala, Wewe hauelewi Ukirsto hata kidogo, Kama unadhani ukirsto ni madhebu umeliwa,
Ninafikiri unashindwa kuielewa vizuri point nilikuwa nimetengeneza. Kwa kifupi tu ni kwamba, Ukristo na Uislam huwa unakufa pale jamii inapokuwa tajiri kielimu na kimaslahi. Historia ya UK inajulikana kabisa kwa jinsi nchi hii ilivyotumia dini kama kiingilio cha utawala wa kikoloni katika nchi mbali mbali hapa duniani. Na katika ukoloni huu, nchi hii ilitajilika kutokana na kuzoa malighafi katika nchi koloni zake.The great success of USA and UK is Biblical, I mean umesababishwa na Nguvu zinazoaminiwa na Wakiristo, sasa unaposema ukirsto ni rafiki wa umasikini sikuelewi.
Mkuu Sangarara sijasema Ukiristo ni madhehebu ila ninachosema hakuna mkiristo duniani asiye na dhehebu. kwa maana kuwa, huwezi kulitenganisha dhehebu na Ukristo.
Ninafikiri unashindwa kuielewa vizuri point nilikuwa nimetengeneza. Kwa kifupi tu ni kwamba, Ukristo na Uislam huwa unakufa pale jamii inapokuwa tajiri kielimu na kimaslahi. Historia ya UK inajulikana kabisa kwa jinsi nchi hii ilivyotumia dini kama kiingilio cha utawala wa kikoloni katika nchi mbali mbali hapa duniani. Na katika ukoloni huu, nchi hii ilitajilika kutokana na kuzoa malighafi katika nchi koloni zake.
Watu waliosombwa na kupelekwa USA kufanya kazi katika mashamba na viwanda walitumia dini kama kujifariji ama njia ya kuponya psychologically majeraha ya kazi ngumu za kila siku kwa kuamini kama Mungu yupo na kuna siku moja kila kitu kitakuwa kama wanavyoamini. Katika kusubiri siku hiyo, ndiyo kila siku waliendelea kufanya kazi ngumu na nzito kuwatajirisha mabwenyeye huku wao wakiendelea kuwa maskini.