Kwanini Ulaya haina majengo marefu kama ilivyo Asia Na America?

Kwanini Ulaya haina majengo marefu kama ilivyo Asia Na America?

CHINA
1695103876870.png
1695108735450.png
 
Unajua maana ya private properties mkuu. Maeneo mengi ya Ulaya wameweka label ya private property. So ni wao kuamua kubaki na hayo majengo ya zamani au Serikali inunue na ijenge mapya. Nafikiria ndiyo reason
 
Londo bridge, kwa msaada wa Wikipedia.

The current bridge stands at the western end of the Pool of London and is positioned 30 metres (98 ft) upstream from previous alignments. The approaches to the medieval bridge were marked by the church of St Magnus-the-Martyr on the northern bank and by Southwark Cathedral on the southern shore. Until Putney Bridge opened in 1729, London Bridge was the only road crossing of the Thames downstream of Kingston upon Thames

Yaani mwaka 1729 tayari walijua hapa kunahitaji Daraja, na Mahali popote kwenye Daraja kama Hilo ni Mji kama Magomeni.

Mwaka 2024 Tanzania Bado hatujaweza kuboresha kingo za mito kama mto msimbazi, Bado tuko kwenye SGR...
Du hatari.
 
Nchi nyingi za Ulaya hazijengi majengo marefu (skyscrapers) kama ilivyo katika nchi nyingi za Asia kwa sababu kadhaa zikiwemo za kihistoria, kitamaduni, za kisheria, kijiografia, na kiharakati za mazingira:

1. Thamani ya Kihistoria na Kitamaduni: Nchi za Ulaya zina miji mingi yenye historia ndefu na majengo ya kihistoria yaliyojengwa katika kipindi cha karne nyingi zilizopita. Kuweka skyscrapers katikati mwa miji hii kunaweza kuharibu muonekano wao wa kihistoria na kitamaduni. Kwa hivyo, kulinda urithi wa kihistoria ni kipaumbele kikubwa.

2. Sheria na Kanuni: Miji mingi ya Ulaya ina sheria na kanuni kali zinazodhibiti urefu wa majengo. Hii ni ili kulinda muonekano wa miji, kuhakikisha inaingiliana na historia ya miji hiyo, na kusimamia matumizi ya nafasi ya anga. Kanuni hizi zinaweza kujumuisha kikomo cha urefu wa majengo ili kuhifadhi skyline na kuhakikisha kuwa majengo mapya hayaathiri vibaya maeneo yenye thamani ya kihistoria.

3. Mazingira ya Kijiografia: Sehemu nyingine za Ulaya zina mazingira ya kijiografia ambayo hayasaidii ujenzi wa majengo marefu. Kwa mfano, miji iliyojengwa juu ya ardhi yenye maji mengi au katika maeneo yenye historia ya tetemeko la ardhi inaweza kuwa na mipaka ya kiufundi na kiusalama inayozuia ujenzi wa skyscrapers.

4. Mapendeleo na Maisha ya Watu: Mtindo wa maisha na mapendeleo ya watu katika nchi za Ulaya yanaweza kuwa tofauti na yale ya Asia. Katika miji mingi ya Ulaya, kuna mkazo mkubwa katika kuendeleza mazingira ya kijamii yanayoweza kutembelewa kwa urahisi, kutunza nafasi za wazi, na kupendelea majengo yasiyo marefu yanayoruhusu mwanga wa asili na uingiaji wa hewa safi.

5. Harakati za Mazingira: Pia, kuna harakati kubwa za mazingira katika Ulaya ambazo zinapigania uendelevu na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi. Ujenzi wa majengo marefu unahitaji rasilimali nyingi na unaweza kuathiri mazingira. Kwa hivyo, nchi nyingi za Ulaya zinahimiza ujenzi wa majengo yanayotumia nishati kidogo na yanayochangia katika uendelevu wa mazingira.

6. Ukomo wa Nafasi: Badala ya kujikita katika kuongeza urefu wa majengo, baadhi ya miji ya Ulaya imelekeza juhudi zake katika kuboresha na kutumia nafasi zilizopo kwa ufanisi zaidi, kutumia ardhi zilizoachwa wazi, na kuboresha miundombinu ya usafirishaji.

Ingawa nchi za Ulaya zina skyscrapers, idadi na urefu wao mara nyingi ni mdogo ikilinganishwa na nchi nyingi za Asia, ambapo kuna shinikizo kubwa la kijiografia na kiuchumi la kutumia nafasi ya juu kutokana na uhaba wa ardhi na idadi kubwa ya watu.
 
Sasa humu wanakuambia majengo makari ni Dubai na China, Waafrica tuna akili za ajabu sana
Hata kamji kadogo kama Ghent, huwezi bomoa yale majengo ya Karne za zamani. We kajenge huko pembezoni. Na unakuta watalii kibao wanamiminika.
 
Kama kiuchumi wako vizuri na wana historia kubwa kwenye mifumo ya maendeleo ya ulimwengu ila ukija kwenye upande wa majengo marefu (skyscrapers) mazuri inapigwa chini na nchi za Asia

Shida nini je, ni utamaduni Wao tu au kuna nini yaani majengo 20 marefu zaidi Duniani hakuna hata moja kutoka Bara la Ulaya.
Hana shida ya makazi
 
Kama kiuchumi wako vizuri na wana historia kubwa kwenye mifumo ya maendeleo ya ulimwengu ila ukija kwenye upande wa majengo marefu (skyscrapers) mazuri inapigwa chini na nchi za Asia

Shida nini je, ni utamaduni Wao tu au kuna nini yaani majengo 20 marefu zaidi Duniani hakuna hata moja kutoka Bara la Ulaya.

Ulaya na marekani ni miji ya medieval time, so ina vitu vya zamani sana. Huwezi linganisha Washington DC au London na Dubai au Hong Kong 🇭🇰.
 
Back
Top Bottom