Aman iwe nanyi wakuu wa jukwaa katika bwana
Kama kichwa cha habali kinavyosomeka hapo juu
Kila binadamu hujiunga mtandao anaoupenda kwa wakati wake na sababu zake kuna wengine hujiunga mitandao fulan ili wapate mademu kwa urahis, wengine hujiunga ili watoe darasa na wengine ili wapige hela, hawa wanaopiga hela wana njia njia nyingi lakin wengi ni kutapel watu
Mimi nilijuanga humu ndan ili nipate kuchangia mambo fulan hasa ya din na siasa na wakati najiunga humu kipindi hicho mijadala ya din na siasa ilikuwa imepamba moto ile mbaya
Wapi niliijulia jamii forum niliijulia mozambiqe nikiwa nimekaa na masela sasa kuna jamaa mmoja alikuwa anajua vitu vingi sana kitendo kilichopelekea nimuulize wewe jamaa mambo haya huyatolea wapi jamaa alilinga kunambia lakin mwisho wa siku alinambia kuwa ni jamii forum hapo hapo nilianza kuitafuta jamii forum na kujiunga mazima
Nawe waweza sema kwanini ulijiunga na wapi kitu gan kilikushawishi
Nawasilisha
LONDON BABY
Sent using
Jamii Forums mobile app