Kwanini ulijiunga JamiiForums na uliijulia wapi?

Kwanini ulijiunga JamiiForums na uliijulia wapi?

One of the best social media platforms ambayo ina constructive ideologies, funny and interesting all the time.

Sababu kubwa ya kujiunga ni kwamba ni jukwaa huru la kutoa/kuchangia mawazo yako kwa kadri ya uelewa wako na pia ni darasa huru la kujifunza mambo mengi kisiasa, kiafya, kielimu, kidini na hata kidunia.
Uliijulia wap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Naamini kila mtu ana kitu au jambo fulani lililo mfanya avutiwe kujiunga na JF.

Kwa upande wangu nilivutiwa na elimu ya mambo mbalimbali itolewayo hapa JF, aidha nilipenda kushiriki mijadala fulani fulani hivi yenye mvuto wa hali ya juu.

Sasa vipi kwa nyie wenzangu, nini kiliwavatia?.
 
Baba yangu ndio sababu haswa, nilikua nikiona anachekelea sana akiwa sebleni akiwa na simu yake , nikagundua anapendelea kuingia jf
 
Baba yangu ndio sababu haswa, nilikua nikiona anachekelea sana akiwa sebleni akiwa na simu yake , nikagundua anapendelea kuingia jf
Kumbe sipo peke yangu ambaye nikikaa na kasimu kangu huku nachat JF, najikuta natabasamu muda wote sababu ya vimbwanga vya JF.
 
Mara ya kwanza jina la Jamiiforums nililisikia Kanisani likitamkwa na Askofu Ngalalekumtwa wakati ule "Taifa limepamba moto" na mijadala ya ufisadi (2007) nikaanza kujiuliza huko JF ndio wapi?
 
kwani kuna social network bora nchini zaidi ya hii??
bila shaka mitazamo chanya ya watu wa JF Ndiyo iliyonivutia mpka kujiunga humu ""na kwakweli pameweza kuikata KIU yangu ..napoikosa huwa najihisi kuwa Nina arosto
 
Mara ya kwanza jina la Jamiiforums nililisikia Kanisani likitamkwa na Askofu Ngalalekumtwa wakati ule "Taifa limepamba moto" na mijadala ya ufisadi (2007) nikaanza kujiuliza huko JF ndio wapi?
Kumbe hata wakubwa nao wapo JF ?, Dah !, Ndio maana unaweza kukutana na Mada au Comments zilizosheheni Weledi na Hekima ya hali ya juu, kumbe ni kwasababu ya uwepo Wa watu wakubwa ktk jamii.
 
Forex ilinifanya nijisajili humu wakati niliifahamu jf tangu 2010
 
Hawa watu walinivutia sana mpaka nikaamua kujiunga rasmi.

Mzizi Mkavu
Kongosho
Bujibuji
Katavi
Mamdenyi
Madame b
Nyani Ngabu
Ila kongosho sijui kapotelea wapi?
Majibu ya Kiranga mkuu yalinifanya nijoin JF2012.
Pasco Mayalla akanifanya nizijue tabia wanaJf.

Serikali ilipoanza kuifuatilia JF ndipo nikajua JF sio UWANJA MDOGO😅😅😅

#KABURI
 
Back
Top Bottom