kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Wengi Tanzania, East Africa, SADC, Africa na Dunia nzima tuliamini Tanzania imejiunga na mataifa yenye umeme mwingi wa uhakika baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bwawa la Nyerere na kuwa kuwa na kiasi kikubwa cha gesi, lakini wapi bwana shida Iko palepale na vilevile. Umeme unaendelea kukatika majumbani, mitaani na maofisini kwa dk 5 na kurudi, nusu saa na kurudi, saa nzima na kurudi, masaa 5 na kurejeshwa na siku nyingine masaa 6 na kurejeshwa.
Umeme kukatika dk 10 na kurudi shida ni umeme hakuna, miundombinu mibovu, au hujuma TU kwa wananchi?
Chama cha siasa legelege huzaa serikali legelege, serikali legelege huzaa mawaziri legelege, mawaziri legelege huzaa wakurugenzi legelege, wakurugenzi legelege huzaa watumishi legelege na watumishi legelege huzaa huduma legelege.
Nataka na mimi kuanza kuamini wale wanaosema CCM ya sasa ni legelege, haishindi uchaguzi kihalali na imeishiwa mbinu na ubunifu wa kisimamia mambo yaende. CCM ndiyo inayozalisha huduma legelege kwa wananchi, imechoka hata kama kusema hivyo ni uchochezi,
CCM imezalisha serikali yenye viongozi na watumishi ambao wanatafuta maslahi nje ya ajira kwa kutumia nafasi za utumoshi wa umma. Kila mtumishi anafikiria atakulaje, atasafirije na atalala wapi kwa mwezi mmoja na baada ya kustaafu kazi au kukoma kwa ajira. Kifupi watumishi wote wa umma wanawaza kupata malipo ya ziada nje ya mshahara kwa kutumia nafasi zao. Hii ni kuanzia mjumbe wa nyumba kumi, mwenyekiti wa kitongoji na mfanya usafi ofisini.
Kwanini umeme uanakatika dk 2 na kurudi, hata hayo matengenezo yamefanyila saa ngapi kwa dk mbili? Mtu atasingizia kunguru na kima ambao wanajulikana kama wapo kabla ya ujenzi wa mradi kuanza. Je, mradi haukuzingatia uwepo wa kunguru na kima wakati wa usanifu?