Kwanini umpe mpenzi wako au mke wako hela mbele za watu??

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,749
Reaction score
62,766
Wakuu kwema??,.

Hivi wanaume wenye hii tabia huwa na shida gani? au ni ulimbukeni? Au nini jamani?

Yaani utakuta MTU wametoka nyumban let say anamsindikiza mke wake stand,. Wakishafika wameshuka kabisaa ndio anatoa wallet anampa hela za kutumia sijui za nini na nini.... Hamuonagi aibu?

Kwanini usimpe kabisa kabla hamjatoka nyumban?, Au labda ndio mmepitia kutoa bank au Kwa wakala haya kwanini usimpe ndani ya gari??..


Yaani mbaba kabisaa na kitambi chako kikubwa mbele ya watu kibao unamhesabia mkeo sijui mpenzi wako hela za kutumia Hadi bible anajiskia aibu maskini,. Lakini atafanyaje sasa anapokea Tu hana namna...

Acheni huu ushamba
 
Fresh tu, na kwa makusudi na mimi nitamuomba hela zaidi hapo hapo mbele ya watu, maana huwa wanaonaga aibu kusema hawana.
 
Pokea hela acha nyodo ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…