Kwanini umpe mpenzi wako au mke wako hela mbele za watu??

Nimeipenda hii

One time kuna home boy alinifanyia huu ujinga

Yeye aliwahi Pata ajira kabla yangu,basi nilienda kumtembelea kwake,basi kanisi dikiza hadi pale kituoni kinondoni b,hiyo miaka kama ya 2011 au 2012

Si tunaagana kituoni eti akatoa msimbazi na kunipa,dah nilijisikia aibu sana lkn nikakausha tu
 
Mkuu ulishajaribu kumpa mumeo pesa mbele za watu ukaona inakuwaje?


Sijui kwanini sioni shida yeyote kwenye hilo maana kila mtu anajua unampa pesa mkeo, ingawa siku hizi wanawake wako very manipulative sana, utasikia hanipi hata mia mimi ndo namtunza wakati ukweli ni vice versa.


Wanaume tujitahidi kuoa wanawake wanaotupenda.

Ni hayo tu kwa leo
 
Kama unaona ni ushamba basi tafuta cha kwako uache kuwa omba omba na tegemezi.
 
Sasa wee unakasirika nini na wakati hela za kwao bwana.....kwanza wenzio hapo wanaseti mitego bwana lazima uattrack warembo
 
Wanawake katika maisha yangu washindwe na walegee siwataki bora nipende hela
 
Ifike muda wanawake mtuheshimu.

Yaani nitafute hela afu mtu aje kunipangia pakumpea, yaani nione aibu kwa hela niliyotafuta mwenyewe.

Kama anaona aibu kupokea hela nitakapompea basi atafute zake.
 
Kwan ni drugs mnapeana? Nikupe Kwa kificho Ili Iweje? Kwan nikikupa mbele za watu wewe unapungukiwa Nini? Na hata nikikupa Kwa kificho inakuongezea Nini?

Tabia kama hizi ndo zile unabeba ndoo yenye maji, unaenda chooni, halafu unataka majirani wajue umetoka kukojoa wakati umetoka kun..ya😏
 
Umenikumbusha mbali sana, kipindi Cha nyuma sana nilikua na boyfriend wa hivyo, yaani kama unasafiri imagine pale ubungo terminal(zamani) nje ya bus ndiyo anafungua wallet anakupa hela watu wote wanaangalia. Nilikua naona aibu sana......anyways gone are those days
 
Ifike muda wanawake mtuheshimu.

Yaani nitafute hela afu mtu aje kunipangia pakumpea, yaani nione aibu kwa hela niliyotafuta mwenyewe.

Kama anaona aibu kupokea hela nitakapompea basi atafute zake.
Jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…