Ni wazi sasa wengi wetu sasa tumeelimika kupitia mada nyingine za hati fungani za NMB (NMB BONDS)ni kupitia mada hizo maswali maoni uchambuzi na hata kuchagiza kwa namna yake vilijitokeza
Wengi waliongelea kuhusu faida kidogo ipatikanayo kwenye hatifungani, lakini naamini kabisa hawakutafakari kuhusu gharama za uendeshaji kodi bima nk za hatifungani
Si kila mmoja wetu ni mfanyabiashara au anaweza kufanya biashara, kwahiyo unaweza kuwaza faida nono unayowaza kupata kwenye biashara fulani lakini bila kutafakari yafuatayo
-kodi za pango
-gharama za uendeshaji
-mishahara ya wafanyakazi
-kodi mbalimbali
-risk mbalimbali
-muda wa ufuatiliaji
Na wakati mwingine hasara au mzigo kuchelewa kutoka kwa wakati
Ukija kuyajumuisha haya yote na faida unayopata utajikuta faida ni ndogo kuliko matarajio yako
Kuna wengi wetu pia wameweka pesa zao nyingi tu bank huku Zikiwa zina makato ya kila mwezi na gharama nyinginezo. .HUKU NI KUPOTEZA
Hivyo basi kwa mkakati huu waliokuja nao NMB wa hatifungani ni wazi utakuwa ni mkombozi kwa watu wengi hasa
wafanyakazi wa kaliba zote
Wafanya biashara kubwa za kati na ndogo ndogo
Watu wa jinsia zote
Wenye kupata pesa za msimu nk nk
Pesa yako ya kunulilia hatifungani inakuwa salama huku ikizalisha
Unakuwa huna pressure hata msimu Unapokuwa chini
Unakuwa huna gharama za uendeshaji
Unakuwa una uhakika wa faida isiyoyumba
Huhitajiki kulipa kodi mbalimbali wala mishahara ya wafanyakazi
Kimsimgi unakuwa na faida yako murua isiyokuletea headache yoyote
Kwasasa NMB ni Benki inayofanya vizuri sana kwahiyo uhakika wa pesa yako unakuwa si wa mashaka mashaka
Hujachelewa bado unayo nafasi ya kununua hatifungani za NMB