Kwanini unasema huna mtaji? Ni kisingizio?

Jamani hii ya kuanza bila mtaji mie ni muumini...kiukweli sio lazima biashara uanze na mtaji..kama ulovyosema mtaji ni kuwa Na muda na akili hili ndo wengi tunafeli hapa!

Sema tukitoa ushuhuda tutaitwa mamotivesheno supika 😒
Wee toa tuu tupate mawili matatu
 

Mkuu ujaelewa nimemaanisha nini hapo...am not your crew in this as you misread my punch.
 

Unaona umenipa kitu hapo. Kwanza hongera sana!!!

lkn nmegundua thamani ya mtaji haichezi mbali na Kujisacrifice pamoja na Uaminifu.

Wacha na mm nianze kutafuta Fursa!!!
 
Nikaanza mtangazia yeye dagaa zake nikapata response nzuri sana bt hakua akinipa % yyt ile.
Possible √√

wakaamua kunipa gunia 2 za asante baadabya miez kaka 3
Ulipewa gunia 2.

Let make word Asante in subset {Asante}.

2.kilimo cha mboga mboga ..niliomba eneo 2015 nilisafishe nilime mchicha ..pemben kulikua na mto fulan haukauk maji bas huy mama akanishangaa itawezekanaje
Possible √√

niliweza lima kwa msaada wa kaka...akanisaifishia akanilimia nikapga tuta nikapata tuta 50
Nataka kujua mbegu, mborea... pembejeo zilizohitaji utoe pesa mfukoni nazo Kaka alisaidia??

nilifunga michezo yawatoto..bas watoto wengi wknd wakawa wanakuja kuomba kucheza...nikaona fursa
Hizi bembea ulizifunga bila kutoa pesa mfukoni??

.......................................................

Bottom line
Nimeenda hand to hand sehemu zitazokulazimu kutoa Cash yako mfukoni, nimepata vitu viwili

1)Ulisaidiwa
*kupewa gunia
*kupewa pembejeo na kaka through kaka umemuelezea kwenye Nguvu kazi tu.

2)Umetoa Cash mfukoni
*All start with bembea last time niliulizia bembea moja used it Satand 70,000 Tzs.
 
Acheni kudanganya watu nyie motivational speakers, hakuna biashara pasipo mtaji ishu tu size ya mitaji inatofautiana hata uo udalali wenyewe mnaokomaa kuaminisha watu hauitaji fedha ni uongo ili kupata wateja unahitaji simu nzuri ya kuchukua content nzuri unahitaji bundle kupost na kuwasiliana na wateja unahitaji kulipia matangazo nknk hizo gharama zote lazima uingie kabla hata kuanz huo udalali wenyewe.
 
Kwenyr mchicha sikuweka mbolea..hilo eneo halijawah kutumika..kalikua kamsitu fulani kenye mbolr...upande wa chinu maji yapo ..mie kilichonivuta ni maji tu ..hata kamA kaka asingesaidia cost yake isingezid 40k .maana ni robo eka kulima sana sana ingecost 20k
 
Unaona umenipa kitu hapo. Kwanza hongera sana!!!

lkn nmegundua thamani ya mtaji haichezi mbali na Kujisacrifice pamoja na Uaminifu.

Wacha na mm nianze kutafuta Fursa!!!
Umeongea point...KUJISACRIFY...UAMINIFU!
 
Mkuu hizi biashara za kwenye karatasi huwa nyepesi sana.
 
Mtu unakuta kaajiriwa anapokea mshahara kila kitu kinaenda. Anakuja hapa eti biashara unaweza kuanza bila mtaji, anadhani watu mtaani wamekaa tu.
Unaweza usiwe na mtaji ukawa na watu ambao wapo kwenye system wakakubeba.
Kuna watu hana mtaji na hana mtu wa kumbeba hapo ndo utajua Pesa ni nini.
Mafanikio sio kitu chepesi kwa 100% ni kitu kigumu sana mpaka mungu akuwekee mkono.
 
Mkuu hizi biashara za kwenye karatasi huwa nyepesi sana.
Mkuu,Hakuna biashara nyepesi ila Kila kitu ni mipango.Niamini kwamba hiyo kanuni niliyompa hapo juu sio rahisi hivyo maana kila hatua hapo ni kazi pevu kabisa
 
Hakuna biashara bila mtaji. Labda tuite kubangaiza ila kama mtaji huna wewe hufanyi biashara na sio mfanyabishara. Kwanza biashara ni nini na ina sifa gani? Ukijibu hili utajua kuwa hakuna biashara isiyo na mtaji.
Mkuu iko hivii, ni kweli kabisa hakuna biashara pasipo mtaji. Lakin neno mtaji ni pana kidogo na zipo aina mbali mbali za mitaji mfano: nguvu (nadhani ushasikia mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe), ujuzi, au hata mali (assets) like kiwanja au nyumba. So, pesa ni aina mojawapo ya mfumo wa mtaji ingawaje pesa inaendelea kusimama km aina ya mtaji wenye nguvu sana kwny biashara!.
 
Ukiwa na haya unaweza kumove on kwa hapa Tanzania:
1. Mtaji pesa kulingana na wazo lako.

2. Knowledge teknolojia/ufundi/fani/ujuzi mfano capenta, welding, seremala, sonara, mekanika, fundi mavazi na viatu, fundi wa electricity na fundi electronics simu, jagi ,pasi, n.k

3.Ukikosa hayo hapo juu au ukiwa huna sifa hizo itakulazimu ufanye kazi za vibarua kama kubeba tofali, kupakia mizigo na kubeba mizigo, kufanya kazi zisizohitaji ujuzi au teknolojia, kufanya kazi za ndani, maids wa bar au hotels

N.B jitahidi utoke kwenye option namba 3 kama unaishi kwa kuangukia hili kundi hapa Tanzania japo ukiwa huna namna sio vibaya kuwepo hapo ili ubangaize ushike option namba 1 au 2.

OPTION 1MTAJI KUTOKA KWA MKOPO, RAFIKI, HIZO MITAJI HUWA NI CHANGAMOTO UMAKINI NI MUHIMU. MTAJI WA KUUKUZA HUO HAUNA SHAKA SANA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…