Ulaya kwenye magari na turbine engines za meli wako vizuri zaidi ya Marekani.
Uingereza walikuwa na Comet ndio ndege yao ya kwanza jet ya abiria na ndio ilianza duniani kama sikosei. De Havilland ndio waliitengeneza miaka hiyo wakiizidi Boeing. Boeing kilichowabeba ni tender za ndege za kijeshi faida walitoa hapo wakawekeza kwa abiria, pia wanakuwa na products ambazo ni dual use ndege inakuwa ya abiria inapewa version yake ya kuwa maritime patrol au anti submarine warfare.
Japan ilitakiwa iwe na uwezo mkubwa wa kutengeneza ndege hasa hawa akina Mitsubishi ila Marekani iliwawekea vikwazo vya miaka 7 kuanzia mwaka 1945 baada ya WW2. Huo muda ndio ulikuwa jet age ambaye hakutengeneza jet miaka hiyo aliachwa nyuma mno.
Ujerumani ilibidi iwe bingwa. Makampuni kama Messerschmitt na Focke-Wulf yalitoa fighter jets kwenye WW2 na zilisumbua. Wao ndio walitoa first jet fighter ikakamatwa na Wamarekani wakaenda kuisoma. Walikuwa vizuri kwenye aerospace engineering hadi rocket la kwanza walitengeneza wao zile V2 flying bombs. Vita iliwarudisha nyuma.
USSR walikuwa na mashindano na Westerns. Designers wao kupitia design and manufacturing bureaus kina KnAAPO na nyingine kupitia wanasayansi wao muhimu ambao wengi walishinda tuzo za Hero of Soviet Union, kina Mikoyan, Mikhail Gurevich, Tupolev, Pavel Sukhoi, Georgy Beriev, etc walikuwa wajuzi sana. Teknolojia ilishindwa kuungana kusaidiana, uchumi ukashuka, emphasis ikawa kwenye ndege za jeshi kuliko rais mwishowe soko la raia ndio kubwa kwahiyo wakashindwa. Hii consortium ya UAC ndio inawabeba hawa watengenezaji wa Sukhoi Superjet-100 ambazo ziko very reliant kwenye tech ya Western. Sanctions zinakuja hawaendi kokote.
UK walitelekeza sekta yao ya anga, wazungu waliokuwa watengenezaji wa spare parts ndio wakaungana kwenye Airbus ambayo mainly ni ya Ufaransa. Washiriki wengine ni UK, Spain, Italy, Germany na sijui kama kuna mwingine. Makampuni kama Aerospatiale na BAE Systems yaliunga juhudi hapo.
Mchina anakopi ila ni vigumu sana kukopi fly by wire systems na vigumu zaidi kukopi jet engines. Hizo wababe ni Rolls & Royce ya Uingereza, Pratt & Whitney ya Marekani. Wengineo ni kina Safran ya Ufaransa, General Dynamics ya US na Aviadvigatel ya Urusi ambayo inaachwa nyuma kwa sababu kadhaa.
Ndege hazina majaribio. Ukiharibu reputation leo kuja kuirudisha hata miaka 20 ni midogo, huwa zinapewa certificate kwa masharti sana hivyo kama hujui kitu usiwekeze hela nyingi mwishoni hakuna atakayenunua. Hata Marekani ilikuwa na McDonald Douglas ikapotea sokoni mpaka ikauzwa kwa Boeing. Ndio watengenezaji wa F-16