Kwanini USA na EUROPE wamelitawala sana anga la ndege za abiria ulimwenguni?

Kwanini USA na EUROPE wamelitawala sana anga la ndege za abiria ulimwenguni?

Taja makampuni mengine ambayo yanatumika duniani kuzidi hayo siyo unakata mauno hapa
Hana alijualo Mkuu ndiyo maana kaishia kudemka tu.Mwenzie anataka kujifunza na wengine kupitia thread hii tunajifunza
 
Hana alijualo Mkuu ndiyo maana kaishia kudemka tu.Mwenzie anataka kujifunza na wengine kupitia thread hii tunajifunza
watu kama hao wanajifanya wajuaji wa kila kitu lakini vichwani hamna kitu
 
Hujajiuliza kwanini Afrika hatuwezi tengeneza hata vifaa vya mashambanj
 
Airbus ni watengemezaji wa ndege kutoka nchini ufaransa , Boeing ni watengenezaji wa ndege kutoka America .
Mara nyingi ndege model za airbus hua zinaanza na letter 'A' , A321 ,A 340 ,A 350 .... et. Boeing wao huwa zinaanza na namba '7' tu , mf 747, 767, 787.
Kuuuuumbeeeeeee[emoji1783][emoji1783][emoji1783][emoji1783]
 
Ulaya kwenye magari na turbine engines za meli wako vizuri zaidi ya Marekani.

Uingereza walikuwa na Comet ndio ndege yao ya kwanza jet ya abiria na ndio ilianza duniani kama sikosei. De Havilland ndio waliitengeneza miaka hiyo wakiizidi Boeing. Boeing kilichowabeba ni tender za ndege za kijeshi faida walitoa hapo wakawekeza kwa abiria, pia wanakuwa na products ambazo ni dual use ndege inakuwa ya abiria inapewa version yake ya kuwa maritime patrol au anti submarine warfare.

Japan ilitakiwa iwe na uwezo mkubwa wa kutengeneza ndege hasa hawa akina Mitsubishi ila Marekani iliwawekea vikwazo vya miaka 7 kuanzia mwaka 1945 baada ya WW2. Huo muda ndio ulikuwa jet age ambaye hakutengeneza jet miaka hiyo aliachwa nyuma mno.

Ujerumani ilibidi iwe bingwa. Makampuni kama Messerschmitt na Focke-Wulf yalitoa fighter jets kwenye WW2 na zilisumbua. Wao ndio walitoa first jet fighter ikakamatwa na Wamarekani wakaenda kuisoma. Walikuwa vizuri kwenye aerospace engineering hadi rocket la kwanza walitengeneza wao zile V2 flying bombs. Vita iliwarudisha nyuma.

USSR walikuwa na mashindano na Westerns. Designers wao kupitia design and manufacturing bureaus kina KnAAPO na nyingine kupitia wanasayansi wao muhimu ambao wengi walishinda tuzo za Hero of Soviet Union, kina Mikoyan, Mikhail Gurevich, Tupolev, Pavel Sukhoi, Georgy Beriev, etc walikuwa wajuzi sana. Teknolojia ilishindwa kuungana kusaidiana, uchumi ukashuka, emphasis ikawa kwenye ndege za jeshi kuliko rais mwishowe soko la raia ndio kubwa kwahiyo wakashindwa. Hii consortium ya UAC ndio inawabeba hawa watengenezaji wa Sukhoi Superjet-100 ambazo ziko very reliant kwenye tech ya Western. Sanctions zinakuja hawaendi kokote.

UK walitelekeza sekta yao ya anga, wazungu waliokuwa watengenezaji wa spare parts ndio wakaungana kwenye Airbus ambayo mainly ni ya Ufaransa. Washiriki wengine ni UK, Spain, Italy, Germany na sijui kama kuna mwingine. Makampuni kama Aerospatiale na BAE Systems yaliunga juhudi hapo.

Mchina anakopi ila ni vigumu sana kukopi fly by wire systems na vigumu zaidi kukopi jet engines. Hizo wababe ni Rolls & Royce ya Uingereza, Pratt & Whitney ya Marekani. Wengineo ni kina Safran ya Ufaransa, General Dynamics ya US na Aviadvigatel ya Urusi ambayo inaachwa nyuma kwa sababu kadhaa.

Ndege hazina majaribio. Ukiharibu reputation leo kuja kuirudisha hata miaka 20 ni midogo, huwa zinapewa certificate kwa masharti sana hivyo kama hujui kitu usiwekeze hela nyingi mwishoni hakuna atakayenunua. Hata Marekani ilikuwa na McDonald Douglas ikapotea sokoni mpaka ikauzwa kwa Boeing. Ndio watengenezaji wa F-16
Mkuu asante kwa kutujuza vitu hivi.
 
Ulaya na USA.Canada, New zealand Australia yaani hawa bana ni wale waleeee!!...Mtu namwanae kamwe hawadhuliani!!....wao hao ndo waanzilishi wenye hati miliki wengine wooote wame copy!

Lazima wakaombe rhuksa kwa wenye Hati miliki...ambao pia wana wapa masharti nafuu km hayo!! kitu pekee alichogundua mchina labda majungu!!...

Ulaya wako ivo ukigundua tu, ng'ombe anaye zaa nyama ya kula basi hiyo ni mali yako mpaka kifo!...utalipwa mpaka unye!...ndo maana mie natamani sana nijue kuruka kwa ungo!! ili niwe na hati milki hii!

Machawi ya africa majinga sana hayajui yakienda ulaya yatakuwa matajiri kufuru...cha kwanza ni kumroga Rais akiwa ikulu alafu anamzindua!
 
Back
Top Bottom