Kwenye usafiri wa anga hakuna siasa wala porojo. Kuna vitu vingi vya kuleta umbea na visingizio ila sio usafiri wa anga ndio maana Urusi na China wote wanatumia ndege za Airbus na Boeing. Ukileta porojo utaua watu hakuna namna hata kama ni unafiki utatumia tu hizo kampuni za adui.
Tunaangalia flight hours tunalinganisha na ajari. Ndege zinazotumika sana zinatakiwa zipate ajari zaidi, IST zinatakiwa zipate ajari zaidi kuliko BMW X6 barabarani. Ukikuta kwa mwaka kuna ajari 100 za IST na ajari 12 za BMW X6 maana yake X6 inapata ajari sana kuliko IST kwa sababu mtaani IST ziko mara hata 50 ya X6, ajari za IST zilitakiwa ziwe mara nyingi kwa namba yake.
Ndege top safest kwenye rekodi utakutana na Airbus na Boeing nyingi na Embraer au Bombardier mbili hivi kwenye top 20. Ukija kwenye ndege mbovu zisizoaminika na zenye ajari nyingi utakutana na makampuni yote ya Urusi watengenezaji: Tupolev, Ilyushin na na Antonov ndege zao zipo kwenye top ten ya ndege zenye rate ndogo ya usalama. Sio maneno ya kutunga, ajari zikitokea si zinaonekana.
Mexico kuna kampuni waliwahi kusema kama wewe "ni propaganda" wakanunua za Urusi Sukhoi Superjet-100 units kadhaa. Hazikukaa hata miaka minne wakazipiga chini zote. Russia kwenyewe waliozinunua ni Aeroflot kampuni ya serikali ambayo ilikuwa na Boeing na Airbus pekee