Kwanini USA na EUROPE wamelitawala sana anga la ndege za abiria ulimwenguni?

Kuna fitna sana kwenye usafiri wa anga maana propaganda nyingi zimewekwa huko
 
Pia nikazie kitu.

Waafrika wengi wanaamini sababu ya Russia kutokuwa na makoloni Africa alikuwa hapendi makoloni, La hasha, Russia alizidiwa mbali sana na Ulaya Magharibi kwenye technology ya kuunda meli, so kwake ingekuwa hasara kupata kuendesha makoloni Africa, pia kuyacontrol kwa haraka
 
Kwenye usafiri wa anga hakuna siasa wala porojo. Kuna vitu vingi vya kuleta umbea na visingizio ila sio usafiri wa anga ndio maana Urusi na China wote wanatumia ndege za Airbus na Boeing. Ukileta porojo utaua watu hakuna namna hata kama ni unafiki utatumia tu hizo kampuni za adui.

Tunaangalia flight hours tunalinganisha na ajari. Ndege zinazotumika sana zinatakiwa zipate ajari zaidi, IST zinatakiwa zipate ajari zaidi kuliko BMW X6 barabarani. Ukikuta kwa mwaka kuna ajari 100 za IST na ajari 12 za BMW X6 maana yake X6 inapata ajari sana kuliko IST kwa sababu mtaani IST ziko mara hata 50 ya X6, ajari za IST zilitakiwa ziwe mara nyingi kwa namba yake.

Ndege top safest kwenye rekodi utakutana na Airbus na Boeing nyingi na Embraer au Bombardier mbili hivi kwenye top 20. Ukija kwenye ndege mbovu zisizoaminika na zenye ajari nyingi utakutana na makampuni yote ya Urusi watengenezaji: Tupolev, Ilyushin na na Antonov ndege zao zipo kwenye top ten ya ndege zenye rate ndogo ya usalama. Sio maneno ya kutunga, ajari zikitokea si zinaonekana.

Mexico kuna kampuni waliwahi kusema kama wewe "ni propaganda" wakanunua za Urusi Sukhoi Superjet-100 units kadhaa. Hazikukaa hata miaka minne wakazipiga chini zote. Russia kwenyewe waliozinunua ni Aeroflot kampuni ya serikali ambayo ilikuwa na Boeing na Airbus pekee
 
Daaah hatari
 
Asikwambie mtu, tecs za US na Ulaya ni za juu saana. Achana na ndege jaribu kucompare products zingine kama magari, mashine za ujenzi n.k utagundua vitu vyao ni jiwe haswa, hawanaga kurahisisha mambo.
Russia pia wanatengeneza ndege za sbiria ila hawajaamua ku base sana huku kuhusu tecs za ndege na anga wapo juu sana us wenyewe wanajua hilo na sababu kubwa ndo mabingwa wa hesabu na physics dunian
 
Mwambie akutajie Russian airplane inayo operate Africa
Umewahi sikia hata rais wa urusi anazuru africap?urusi hawana maslahi kabisa na africa kwa sababu wana natural resources nyingi kuliko nchi yoyote duniani so hawana cha kufuata huku besides kwani nilazima kuwa na biashara ya ndege kama taifa?
 
Maswala ya anga mrusi anategemea usa rudi shule kwanza hujui lolote
 
Asikwambie mtu, tecs za US na Ulaya ni za juu saana. Achana na ndege jaribu kucompare products zingine kama magari, mashine za ujenzi n.k utagundua vitu vyao ni jiwe haswa, hawanaga kurahisisha mambo.
Upande wa ndege za abiria Asia bado hawaja improve.Ila upande wa electronics,magari na vifaa vya ujenzi tusiongopeane JAPAN IS THE LEADING ONE IN THE WORLD.
NA KWA ELECTRIC CARS NCHI INAYOONGOZA NA S.KOREA.
 
[emoji1544][emoji1544][emoji1544]Mkuu kwanini tusianzishe uzi unahusu ndege uwe unatupa madini.
Mtaalamu wa mambo ya ndege humu JF ni barafu ambaye bahati mbaya miezi zaidi ya nane sijamuona sijui nini kimempata. Mimi hapo nilidokeza tu wala sio utaalamu wangu nimejua hasa kutokana na kufuatilia ndege za kijeshi, makampuni yanayotengeneza ni almost yaleyale.

Kingine mimi ni plane spotter hivyo inanisaidia kujua mambo kadhaa kuzihusu. Naweza iona angani nikajua ni aina gani zile common
 
Boeing na Airbus share one thing in common , Jet engines
Warengenezaji wa engine hiz wapo europe. na America, na wameziwekea pattents na copyrights,
America wana pratt &whitney, pamoja na General electrics, europe wana rolls royce
 
Tatizo lugha, asilimia kibwa ya Warusi hawajui English kwa hiyo propaganda zao haiwafikii wengi
 
Jamani kuuliza si ujinga kwani Airbus na Boing tofauti yake ni nini?
Airbus ni watengemezaji wa ndege kutoka nchini ufaransa , Boeing ni watengenezaji wa ndege kutoka America .
Mara nyingi ndege model za airbus hua zinaanza na letter 'A' , A321 ,A 340 ,A 350 .... et. Boeing wao huwa zinaanza na namba '7' tu , mf 747, 767, 787.
 
HIZI HABARI UMEZITOA WAPI AU ULIMSIKIA MTU AKIZUNGUMZA NDO UKAJA KUULIZA JF
 
Kuna fitna sana kwenye usafiri wa anga maana propaganda nyingi zimewekwa huko
Wabongo bhna.kama fitna mbona hujiulizi mbona hao Russia na china bado wana nunua na kuagiza izo boing na Airbus sometime lazima ujiulize au uulize maswali Kwa wataalam kabla ya kulaum.mfano hao hao boeing na Airbus wate injini Wana nunua Kwa Kwa mwingeleza kama Kam ingikuwa fitna tungeona mwingeleza nae anatengeza ndege zake maana part muhim zinatoka kwake.
 
HIZI HABARI UMEZITOA WAPI AU ULIMSIKIA MTU AKIZUNGUMZA NDO UKAJA KUULIZA JF
Mwenzio kaleta mada tena kawa specific kabisa anataka kujuzwa,wewe badala umjuze kama una uelewa unaishia kumwandikia comment yenye uppercase ambayo ni dalili ya kupiga makelele.Huoni wenzio wenye uelewa na haya mambo wanavyotiririka kutoa kile walichonacho.Kama hujui kitu ni bora uwe msomaji kimya kimya pia ujifunze,siyo dhambi.
 
190 something wright brothers walitengenesa ndege ya kwanza walikuwa ni wamerikani ..
 
Umewahi sikia hata rais wa urusi anazuru africap?urusi hawana maslahi kabisa na africa kwa sababu wana natural resources nyingi kuliko nchi yoyote duniani so hawana cha kufuata huku besides kwani nilazima kuwa na biashara ya ndege kama taifa?
hv unahusi marekani hawana natural resources nyingi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…