Kwanini utajiri wa Elon Musk anashuka sana?

Kwanini utajiri wa Elon Musk anashuka sana?

Biashara kubwa ya Elon Musk ni magari ya Tesla.

●Hisa za Tesla zomeshuka kwa kiwango kikubwa sana zaidi ya 60% wawekezaji wamepunguza ununuaji wa hisa

●Sababu ya pili ni ushindani mkali kutoka kwa kampuni ya China ya utengenezaji wa magari ya umeme ya BYD ambayo kwa sasa imeizidi Tesla kwenye mauzo

Kuna uwezekano Musk akapunguza 10% ya wafanyakazi wake kwenye viwanda vyake vya magari ya Tesla kwa sababu ya kushuka kwa demand
Hongera mkuu umechangia kitafiti kabisa
INGAwa jamaa alikuwa na mpango wa kufungua kiwanda kikubwa kichina sijui ilikuwaje
 
Tesla stock imeshuka sana, na sasa wamesema cybertruck zote zilizouzwa zirudishwe zina shida ya pedal ya kuongeza mwendo wa gari.
EVs za Mchina zinaua soko la Tesla hadi Tesla wanalazimika kushusha bei ili wauze. Mauzo yameshuka sana pia. So, Elon is taking a deeper Dive
Duh hii ilitokeaje mistake kubwa Sana
Mbona jamaa ni smart sana
 
Duh hii ilitokeaje mistake kubwa Sana
Mbona jamaa ni smart sana
Mkuu kawaida mbona tu magari mengi huwa yanakuwa called back viwandani, si toyota, si merecedes, si Nissan. Tesla stock yake ilikuwa ina thamani kubwa kwa sababu inachukuliwa kama tech company kuliko automobile company. Mchina ana zaidi ya makampuni 200 ya EVs na wanauza EVs zao cheap na ziko backed na serikali huko Ulaya wanataka zuia maana zinaua soko.
By the way miaka yote gari za Tesla zinalalamikiwa kwa kuwa na makosa ya finishing, hawako makini sana kwa kila detail. Lakini hii ya pedal ni kosa ambalo linahatarisha maisha ya watu. Pedal inaweza kugomea chini inamaana gari full mbio.
 
  • Thanks
Reactions: FWC
Hongera mkuu umechangia kitafiti kabisa
INGAwa jamaa alikuwa na mpango wa kufungua kiwanda kikubwa kichina sijui ilikuwaje
Nchini China katika jiji la Shanghai ana kiwanda kikubwa sana cha kutengeneza magari cha Tesla

Ilikuwa leo aende India kukutana na PM wa India Narendra Modi. Ilikuwa aende kutangaza kufungua kiwanda kingine cha magari ila amehairisha safari ya kwenda India

Wadadisi wa mambo ya kibiashara wanasema huenda alitaka kufanya hivyo ili kuwaboost wawekezaji wanunue hisa zaidi
 
  • Thanks
Reactions: FWC
Back
Top Bottom