Kwanini utajiri wa watu wa Nyanda za juu Kusini, huwa hauchechemui watu?

Wewe ni mmoja wao au mnufaika, anza kujipanga mapema, mwisho uko karibu!
 
Ratiba yako leo Mbeya inasemaje?😀😃
Nitakuwa NASOMA bar braza...
Sema hapa nimeamka kidogooo niko ""Ovesiiii""

Halafu pale NASOMA kwa nje kuna mdada mweupe ana saluni, mtoto mtamu balaaaa.
Nikifika pale nitajifanya napita nje ya saluni yake ili anione, aniite, nimpigishe bia, tukumbushie ile yangu mimi na yeye..!!!

#YNWA
 
Acheni ndagu jamani,hata habari za Mungu na shetani umesimuliwa
 
Huko usukumani niliwahi kumuelekeza jamaa mmoja utaratibu wa kazi fulani inavyofanyika ye akawa analazimisha utaratibu uvunjwe nikaona anataka kunipanda kichwani nikampiga mkwara mzito sana sasa wadau kibao wakawa wananishangaa kumbe bana nampiga mkwara tajiri mmoja mkubwa

Tatizo alikua hafanani na utajiri alafu mgumu kuelewa kichwa kigumu kichizi yani.
 
Majitu makubwa lakini yanaamini kuna utajiri wa kichawi! Ukimuona mtu mtaani unaweza kusema ana akili, kumbe kichwani anaamini kuwa kuna kuku anadonoa punje na kukupa utajiri!!
 
Nakataa. Wakinga walikuwa na hela siku nyingi ila walikuwa hawajui. Wana kaushamba flan na wanamfumo wao wa maisha tofauti na wabongo wengi ni wabahili ila wana malengo mazuri. Uchawi sikatai kila kabila hawakosi. Kumbuka mkinga una duka karibu nae lakin kwao ana shamba la miti. Miaka hiyo tunaenda minadan na tugimbe ukiambia ndio huyu hutaamin.
 
Miti inawatoa sana wakinga ila watu wanasema ni wachawi
 
Akili za watu wenye kipaji cha ufukara ndo hizi.Utakufa ukiwa maskini wa kutupwa.
 
Kwa kifupi Wakinga wanajua kutafuta pesa,lakini hawajui kutumia.
Na hiyo ndiyo kanuni ya kutajirika; ukiingiza 1000,tumia 200 na 800 wekeza au save.
 
Kwa zaidi ya miaka 15 niliyoishi na kufanya shughuli zangu mikoa ya nyanda za juu kusini nakubaliana na wewe kabisa. Matajiri wengi ninaowafamu binafsi (wengine ni marafiki zangu) wana nidhamu kubwa sana ya pesa, hakuna hata senti moja yao inayochezewa. Hawa ni watu waliokuwa hawana kitu 15 years ago, sasa hivi wako mbali sana, siri kubwa ni nidhamu ya pesa na kujituma. Hayo ya pesa za punje za mahindi ni blabla za kujifariji tu.
 
Wakinga nimeishi nao Mbeya kuanzia niko mvulana hadi nazeeka. Ukitaka nikutajie matajiri wa zamani halafu na wewe uniambie mali zao ziko wapi??

Siyo mnabisha tu wakati mkoa wa Njombe ndiyo unaongoza kwa ushirikiana wa kupoteza watu.

Juzi hapa mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka unajuwa alisema nini kuhusu tajiri ana milioni 600 Benki lakini anaishi maisha magumu hadi kupanda bodaboda.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…