Japkas
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 3,011
- 4,617
We jamaa unanichekesha sana. Inaonekana kuna kitu mmetofautiana na Mkinga mmoja kuhusu pesa.Utakuwa na wewe ni mmoja wapo. Kazi kuchapa wanachapa makabila mengi tu ila nyinyi mumeongeza na uchawi wa makafara. Sasa kama nyinyi ni matajiri kwanini hamuishi maisha ya starehe kama Wachagga?? Wachagga wwnapiga kazi, wanatunza hela lakini kwenye matumizi bado ndiyo kabila linaongoza kula bata.
Waangalie Wachagga Desemba wanavyondoka na magari ya fahari kwenda Kilimanjaro. Wanafanya sherehe, wanakaa kwwo kwenye majumba mazuri.
Nyinyi Wakinga bado Makete iko kama enzi za Nyerere. Mnamiliki magorofa Kariakoo, Mbeya ma Iringa lakini Makete hakuna kitu.
Acheni USHIRIKINA
Ushirikina upo ila haukufanyi uwe tajiri wa kutupwa. Fuatilia wakinga wote kama ni wavivu wa kufanya kazi na kusubiri pesa za ushirikina. Hawa jamaa wanapiga kazi balaa. Kwao kutoendelea kuna sababu nyingi zilizosababisha ikiwemo Elimu kuchelewa kufika kuliko mikoa mingine.
Wengi wa vijana wa kikinga wa leo wamepata utajiri kupitia misitu ya mbao waliyoachiwa na babu zao. Fuatilia Mbao nyingi nchini zinatoka wapi hapa nchini.