Niwakumbushe tu Wakinga siku hizi wanapeleka watoto wao shule nzuri. Na mfumo huu ulianza mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000. Wakati huu baadhi ya wazazi waliwekeza kwenye kupanda miti kwenye maeneo yoye yasiyo na rutuba kwa mazao wakiendelea kuwasomesha watoto wao kupitia biashara wanazofanya. Miaka hiyo ya nyuma ilikuwa ngumu kuwakuta wakinga kwenye taasisi za serikali au binafsi kwa wingi kama ilivyo kwa Wanyakyusa, Wachaga, Wahaya na makabila mengine ukiachana na yule mzee wa degree kumi na mbili Tuntemeke Sanga. Huyu mzee ndiye aliyesisitiza umuhimu wa Elimu kwa famiĺia za kikinga.
Watoto hawa wa Kikinga wamesoma mpaka vyuo vikuu nchini na ughaibuni. Walipomaliza masomo yao ndio tumepata jamii ya vijana kama Mbunge Festo Sanga, Fred Vunjabei kutia ndani kaka zao waliowatangulia pamoja na wadogo zao ambao wametapakaa kwenye taasisi mbalimbali za elimu. Kizazi hiki kinafanya biashara tofauti na wazazi wao. Hawa ni wa kidigitali. Kwa sababu ya elimu wanafuata mzigo China na Dubai na kuja kutulangua nchini. They are making big money kutokana na mtaji waliochiwa na wazazi wao. Jaribu kufikiria deal la vunjabei na Simba bila figisu angekuwa anatengeneza pesa kiasi gani.
Uchawi na pesa ni ujinga mtupu. Kama ni mvivu na huna self controls ya matumizi ya pesa hata upewe pesa kiasi gani utakuwa maskini wa kutupwa tu. Wakinga wanainvest on both formal and informal education kwa watoto wao.