Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwakweli hizi kazi mtu umeusubiri placement umechekelea unajua ushamaliza,unakaa Tena kwa stress unasubiri uitwe dah..hapo ukitoboa adult nenda tu sidhani kama kule michakato itakua mirefu hivyo,shida ni kwamba endapo utakua ushaingia kwenye mfumo tayari
 
Nitawaeleza hao adult Kila kitu then wao watanishauli cha kufanya
 
Kwani process kuwa ndefu nitatizo la taasisi au ndivyo ilivyo tu?
 
Labda hiyo michakato kuna mambo mengine
Mchakato ni mkubwa lazima wahakiki vyeti wao na mamlaka husika kama TCU au NACTE pia taarifa zako za benki na vitu vingine kibao so inachukua mda nikihesabu tuliopata kazi wa fani tofauti zote Zaid ya watu mia so kazi ni ngumu mkuu pia ipo hivyo karibu kote Kuna mdau nilikutana naye huko nikachukua namba yeye ni ofisini ya wilaya ndo walitoa kazi naye mpaka tarehe 24 nilichek anasema alienda wakamwambia asubiri watampigia simu
 
duuuh aseeh kweli kupata kazi ni kazi pia
 
Kada Gani bro
 
Hili la tano hata layman wa sheria anaweza tembea nalo
 
Hebu niulizie kwa prok yeye ana experience marafik zake walipata kazi halmashauri na TRA Atuambie walitumia mda gan mpka kuanza kazi
Kwa nini akuulizie wakati nipo hapa[emoji3]. Wale wa TRA walianza na training haikuchukua muda, aliepata halmashauri sehemu ilikuwa vacant kabisa so mwezi wa 12 ilibidi aende kufanya kazi na hayo mambo yakusubir check no alikuja kupata mwezi wa pili mwanzoni kama sikosei. Mastate attorney wa juzijuzi mwezi wa saba sijui wa nane walivyochukua barua waireport kazini within 2 weeks ilivyotakiwa na washaanza kazi ila sijui malipo inakuwaje,, mimi nahisi hii pia inategemea na uharaka wa kumuhitaji huyo mtu, mfano mastate attorney karibia wote hadi wale wa parliamentary draftman wameazimwa na NPS mpaka mwezi wa kwanza maana NPS hawakuwa na watu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…