Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Pia,..Ungefunguliwa uzi maalumu kwaajili ya hii mada, itasaidia.
 
Nimefungua uzi kule kwenye jukwaa la siasa (maana ndiko waliko wanasiasa wanataka kuwatenga wengine kwenye ajira). Uzi wenyewe unasema:

HUU UBAGUZI WA NSSF HAUKUBALIKI: Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "wa ndani" humo NSSF. Rais SAMIA ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!!​

Naomba wadau wote waliopo kwenye uzi huu tutumie uzi huo kwa nguvu zote kupinga huu ubaguzi. Kila mmoja atie neno hapo, ili ndani ya siku chache kuwe na mamilioni ya views na malaki ya posts zinazopinga ubaguzi kwenye ajira. Nina uhakika watalazimika kubadili msimamo!!
 
Suala la viongozi wakubwa na wakurugenzi kufai waajiri wenyewe ni kwamba kwanza wanandg zao wanashindwa kuwapachika katika kazi, pua kulega kwa Psrs mara kuvuja paper mara kuchelewa mchakato nayo sababu nyingine kubwa, ila hapa tulipo fikia saizi ndio zama za fungulia mbwa yaani hapa saiz kiukweli pagumu kwa watu wa chini kupenya huko.Mwenye uwezo wa kuweka sawa hili ni kiongozi mkuu, kama magu aliweka sawa gii issue bora na yeye alikaushia vibali kuliko vibali vitoke kazi ziishie kwa watu wa kupenyezewa
 
Safi sanq mkuu
 
sisi tunawalalamikia Nssf lakini ukweli ni kwamba Nssf kajilipua kuwa liwalo na liwe ,ila alichofanya Nssf ndicho taasis nyingi inatekeleza behind the scene

umasikini ni laana wazee nchi imegeuka kuwa ya kundi la watu wa tabaka na ukanda fulani
 
sisi tunawalalamikia Nssf lakini ukweli ni kwamba Nssf kajilipua kuwa liwalo na liwe ,ila alichofanya Nssf ndicho taasis nyingi inatekeleza behind the scene

umasikini ni laana wazee nchi imegeuka kuwa ya kundi la watu wa tabaka na ukanda fulani
Inaumiza sana mwanangu Mfwende ,we mwenyewe nadhani unajua Madudu uliyoyaona kwenye zile kazi za majeshi .
Tegemeo la wengi ilikuwa ni huku kwenye huku PSRS ,sasa nako wahuni wanavuruga na kutaka kutengeneza mifumo yao ya kihuni .
Hii trend mbovu kichizi mazeee ,
Zinatengenezwa tabaka hapa
Mbaya sana hii
 
sisi tunawalalamikia Nssf lakini ukweli ni kwamba Nssf kajilipua kuwa liwalo na liwe ,ila alichofanya Nssf ndicho taasis nyingi inatekeleza behind the scene

umasikini ni laana wazee nchi imegeuka kuwa ya kundi la watu wa tabaka na ukanda fulani
Na kajilipua kwa sababu anajua kuna vigogo viko nyuma yake!! si kwa jeuri hii. Lakini Mungu wetu ni mkubwa na ni mwenye haki, huu ubaguzi hautafanikiwa!
 
Kuna watu naona wanalalamikia watu wengine kujitolea. Watu kujitolea sio kwamba wanapenda bali hali ya maisha inapelekea mtu kuamua kujitolea, Just imagine mtu kaomba kazi privates zaidi ya 80 anakosa, anaamua kuomba kazi Serikalini anakosa, wakati huo huo anahitaji kujitimizia mahitaji yake madogo madogo. Mtu huyu inafikia hatua anaamua kwenda kujitolea tu kwa Taasisi au shirika lolote litakalomkubali ili aweze kuondokana na aibu ya kukaa mtaani bule au aibu ya kuomba sabuni au mafuta kwa ndugu.
 
Watu hawa lalamiki juu ya kujitolea wanacho lalamika ni namna gani hizo nafasi za kujitolea zinavyotolewa, umesha wahi kwenda kuomba nafasi za kujitolea kwenye hayo mashirika ukakubaliwa? ukienda kuna majibu mawili makuu utayapata
1. Nafasi ya kujitolea hakuna
2. Nenda kaandike barua utuletee (hapo ni pale umemkuta aliyekupokea siku hiyo ni muungwana), unaileta barua unakaa kusikilizia majibu ,siku, majuma, miezi , miaka inakatika , barua imetupwa kwenye dustbin habari inakuwa imeishia hapo.
 
Mimi kupata INTERN nilipitiaTAESA . Nilifanya Interview nikapangiwa INTERN pale TRA, nikakomaa kwa miaka miwili. Mkataba ulipoisha tukaondolewa wakapatiwa vijana wengine nafasi ya INTERN. Ilikuwa mwaka 2020 hadi 2022. Ni utaratibu mzuri sana ambao unawapa vijana kuongeza CV yao.
 
Usilolijua ni kwamba hizo nafasi za kujitolea kwenye baadhi ya taasiosi, ni neno tu kujitolea lakini kuna posho ya kueleweka tu!! Na huwezi kuipata nafasi hiyo ya "kujitolea" bila connection. Na kujitolea huko ni hatua ya mwanzo tu ili kuhalalisha ajira hapo baadaye!! Ndiyo maana kuna makelele ya vigogo kutaka "wajitoleaji" wapewe kipaumbele!! Je ni lini ulisikia tangazo la kazi za mikataba au za kujitolea huko NSSF?
 
Umesema kweli kabisa!!
 
Watu walioingia huko kwa jinsi yake ni wachache sana dhidi ya wengi walioingizwa huko kwa connection. Na nyie wachache hutumiwa kuwafumba watu macho!! Lakini hata hivyo, hoja ya msingi ni kutaka kuwatenga waombaji wengine walio nje ya NSSF kwa sasa!! Hao ma-intern wasiepushiwe ushindani kwa kuwatenga na kuwazuia waqombaji wengine!!
 
Dah ila mama ktk hili kashauriwa vibaya so sad kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…