Ni kweli ndio maana mashirika na taasisi za Serikali zimekuwa ni mzigo kwa Serikali hii ni kutokana na Manpower iliyopo kuwa imeingia hapo za kwa vigezo vya uwezo bali ni kujuana pia hakuna anayeweza kumchukulia mwingine hatua kwa sababu ya kujuana huko, mwisho wa siku ni haya mashirika kuperform chini ya kiwango ili hali kulipana mishahara minono na marupurupu ndio kipa umbele.
Serikali inatakiwa kulitazama jambo hili kwa upana sana , hili la NSSF limeshtua sana, inatia shaka hata huo usaili wa TRA wa wiki ijayo unaweza kuwa ni kutimiza taratibu tu watakaopata ajira ni haohao waliopo TRA wanaojitolea.
Fikiria tu kwamba , mwezi wa kwanza vijana takribani 700 walifanya oral upande wa Tax management officer kati ya hao 184 ndio walioitwa kazini, kwa hiyo inaonesha vijana wengi kati ya idadi hiyo walikuwa data base ya utumishi, sasa swali ni kwanini isengetumika busara kwa hizi nafasi za sasa 206 za tax management officer kuwapa vijana waliokuwa data base ya utumishi ,kisha wakati ujao ndio hawa TRA wangeendelea wenyewe na mchakato wao wa kuajiri., ukizingatia kuwa hawa vijana waliingia data base mwezi wa kwanza na TRA wametangaza kazi mwezi wa tano, takribani ni miezi 3 tu ambayo kwa life span ya data base ilikuwa bado sana.
Ndio maana nikiitazama hii hali naona kuna jambo nyuma ya pazia.
Nampongeza sana Mh. Rais Dr. Samia Hassan kwa kufungua fursa za ajira nyingi sana kwa vijana kipindi hiki cha uongozi wake, ila changamoto hii aitazame kwa jicho jingine kabisa kama kuna watu wanamshauri ndivyo sivyo ni vema akapingana na mawazo yao maana itamharibia kazi yake nzuri aliyoianzisha ya kufungua fursa za ajira kwa vijana.
Jambo muhimu ni kuwa ajira zitangazwe watu waombe wakashindane , atakaeshinda apate nafasi lakini siyo kama ilivyojitokeza hili la NSSF limeta taswira mbaya sana kwa taifa.