Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ni suala la muda tu, utalamba asali na ushuhuda wako utawatia sana nguvu wengine!
 
Mbona nasikia huko kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UNA) watu wanakula sana maisha mkuu.
Inategemea alikuwa akifanya kazi wapi...!!

Sisi wengine bado tupo tupo huku mashirikani taking some green pasture na bado mambo yananyoka kwa kiwango chake.

Binafsi niliwaza kuja kuwa mtumishi wa GoT at my 40 when everything is OK 😋 and that's what I always think of.
 
Jamani Mwifwa Twinawe na wengine na naomba kuuliza swali mwajiri anapokuambia urudi nyumbani baada ya kureport kazini alafu mwezi na wiki vinakatika bila kuitwa hii inakuwa na tafsiri gani?
Je kabla ya kuondoka ulijaza form ya taarifa zako pamoja na akaunti yako? Kama ulijaza wala usiwe na wasi wasi utakula mishahara ukiwa nyumbasni kama wakichelewa kukuita!
 
Watu hadi wanaonekana kukata tamaa kabisa humu
Ni muhimu sana kutokukata tamaa!! Kukata tamaa hakujawahi kumsaidia mtu yeyote!! Si vizuri kufanya kitu ambacho hakijawahi kumsaidia mtu yeyote!! Pitia shuhuda za watu humu waliovumilia kwa muda mrefu lakini hatimaye wakalamba asali!! Hii itakutia sana nguvu! Kumbuka pia kuwa Mungu ni mwaminifu, na ndiye mtoa riziki kwa watu wote, ni suala la muda tu!!
 
Hakuna stress mbaya utumishi kama kusubiri placement ya ajira..

Nani ameshawahi kupitia hii hali wakuu ?

Ndugu yangu pole, nakuelewa unachopitia.

Lakini umeshawahi kumuwaza na mtu aliyesoma kitu ambacho ajira zake kutoka ni ndoto!? Yani yeye hata tukio lakuona Serikali imetangaza nafasi ya alichosomea ni sherehe, anaweza kukaa mpaka miaka miwili haijawahi kutokea nafasi ikatangazwa na endapo akipishana nayo, itambidi asubiri sana.
 
Mungu ni mwema, wadau na mm leo nimelamba asali namshukuru sana mungu, nawashukuru wana uzi huu kwa faraja zenu kipindi nasubilia placement wadau msikate tamaa wakati wa mungu ndio wakati sahihi, lakn pia naamini yajayo yanafurahisha kwa upande wenu.
Hongera sana mkuu. Mungu azidi kukusimamia ktk majumu yako mapya.
 
Mungu ni mwema, wadau na mm leo nimelamba asali namshukuru sana mungu, nawashukuru wana uzi huu kwa faraja zenu kipindi nasubilia placement wadau msikate tamaa wakati wa mungu ndio wakati sahihi, lakn pia naamini yajayo yanafurahisha kwa upande wenu.
Mwamba rinyungu,hongera sanaaa aseee
 
Mkuu mie namshukuru Mungu nimepass aptitude test,na nimeitwa oral bot,nimeomba likizo ya wiki 1 job,saiv Niko chimbo najiandaa na oral,dua zenu muhimu🙏🙏🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…