Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Asante kwa ushauri mzuri.

Course niliyosoma inahuhitaji mkubwa sana kila siku wanaajiri watu.

Nimejiwekea asilimia kubwa za kupata kazi .

Ila mambo mengine namwachia Mungu.

Nimeshaanza kudharaulika mjini.
Kudharaulika ni GIVEN hiyo kwa jobless nakumbuka nilihama mji niliozaliwa baada ya kumaliza chuo bila hata kupata ajira nikaenda kujilipua mbele huko maana vijana waliofeli form iv nilikuta wanamaisha mazuri sana baada ya mimi kumaliza chuo.

Jobless lazima upitie tanulu la moto likufundishe maisha ni nini.
 
Jobless wa Mungu.Mungu awatangulie mpate kazi sisi tuko private tunalamba asali kiaina.

Kipind nipo jobless ndonilijua mwanaume kukosa kazi ni hatar hata home respect amna ila ukilamba asali respect inarudi.
 
Wakuu jobless tunateseka San imagin unamfata mtu akusaidie[emoji24] anakup maneno si mazuri hayan afya mood yako ya siku inapotea kabisa anakuambia upamban dahh ova[emoji24][emoji24] na familia masikini Hain msaada wowot aisee yasikie tu unafahamishwa mtu mfuate huenda atakusaidia unajitambulish vizur yy anakutoa ktk mood tuombeane wakuu watu wamebadilika
 
Mkuu haya yote yataisha ni suala la Muda Tu mkuu, Ipo siku tutatoka kwenye huu ujobless, uvumilivu unahitajika kwa umakini mkubwa sana. Nyakati ngumu hazidumu ni mapito Tu yataisha haya mkuu
 
Pole Sana aisee yote Ni mapito,siku moja yatabakia kua historia
 
Wakuu na vijana wenzangu wasaka asali, Kijana mwenzenu nilichoka private sector na kuhamasishwa na thread hii ya JF kutafuta ajira serikalini.

Kwa mara ya kwanza application yangu ikafanikiwa na kuitwa kwenye usaili pale Udom (written), licha ya nyomi na baridi ya kufa mtu Mungu akanisaidia kuitwa na oral pale Rose migiro.

Swali langu, Acc yangu kwenye Web na App vinasoma SELECTED for Oral.. ila nataka kufahamu kama vina uhusiano wowote na oral niliyopiga?

Mwisho nawatakia heri na baraka wasaka asali wote.. Mungu ni mwema tuendelee kusubiri maana ni Mwaminifu na humpa kila amwombaye. Amen.
 
Hongera sana je ulifanya taasisi gani? uhusiano upo kwa tafsiri isiyo rasmi umefaulu usaili yaani upo katika kundi la waliopata juu ya 50 oral, kwahiyo itategemea taasisi uliyofanyia usaili inataka watu wangapi na wewe kati ya hao mliofanya oral na kupata 50+ wewe ni wangapi, kama taasisi wakiita watu kazini na usipoona jina lako ujue walioitwa walikuzidi maksi hivyo utabaki database kwa muda wa miezi 12 kusubiri bahati yako .
 
Mkuu haya yote yataisha ni suala la Muda Tu mkuu, Ipo siku tutatoka kwenye huu ujobless, uvumilivu unahitajika kwa umakini mkubwa sana. Nyakati ngumu hazidumu ni mapito Tu yataisha haya mkuu
Kabisa mkuu yaan mpk sasa maumivu ninayo nayakumbuk maneno yake dahh jmn binaadam lazim tusaidiane hata km upo ktk cheo ni jambo la mda tu hujui Nan atakaekuj kukufaa kesho yak inawezekan huyo jamaa yko uliemsaidia akadharau lkn yule wa mbal akasaidia
 
Mambo ya Status hata kama yana maana yake, binafsi nakushauri uendelee na mishe zako wala usihangaike nazo kabisa.

Baki tu kufuatilia PDF ya placement kuanzia miezi 3 mbele tangu tarehe uliyofanya oral.
 

Shukrani Mkuu, nilifanya oral za MDA’s. Ngoja tuendelee kusubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…