Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ukiona wamepost ujue mambo yote yaliyochini ya himaya yao yashakamilika, kama wameirudisha PDF huenda wanakamilisha mambo yaliyopungua/sahaulika.
 
Huenda ni human error labda Muda wa kuyatoa ulikuwa bado..
 
KIUKWELI KWA HII MKEKA ILIYOTOKA JANA INA WATU ZAIDI YA 600+

nadhani wasubiri mikeka tujipe wiki mbili za kupumzika.

Maana masjala ya wazi itakuwa busy sana wiki ijayo .
 
Yah Jana saa nne IT aliweka.mkeka tofauti na huu akaufuta ndo amekuja kuupost huu leo.

Ulikuwa na watu zaidi ya 200
Mkeka wa watu zaidi ya 200, upo na umepostiwa jana.

Wahusika Hongereni sana, mnaenda Masijala mkiwa na Tabasamu kabisa tofauti na siku ya Oral mlipopita pale nje (Masijala) ambapo presha ya mkando ilikuwa juu[emoji23][emoji23]
 
Hongera sana mkuu,

Nakutakia uwe na mafanikio katika kazi yako, katende haki na kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.

Furahia jambo hili ukiwa na ndugu na jamaa zako wa karibu ili kuweka kumbukumbu kwan haikuwa rahisi mpka kufika hapo.

Pia, kumbuka kutoa Shukrani kwa watu wenye uhitaji kutoka katika mazingira yako.
 
Wazima,ndugu zangu ..first experience kuhusu utumishi nilipata humu na ndo ilikuwa first interview hatimae Leo nimepata placement ..Mungu ashukuriwe ..alieanzisha huu Uzi uzidi kubarikiwa

Hongera sana mkuu,👊👊

Huu uzi umebarikiwa sana, ukipita humu na malengo yako lazima utoboe. Ni suala la muda tu.

Karibu sana katika Utumishi wa Umma, zingatia kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni unapotimiza majukumu yako na pia katende haki.

Furahia mafanikio haya pamoja na ndugu na jamaa zako na pia kumbuka kutoa Shukurani hasa kwa kusaidia makundi yenye uhitaji katika mazingira yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…