Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Wakuu msaada kidogo, kwa wale tuliyolamba asali na tuliripoti kituo Cha kazi mwanzon mwa mwezi huu, na tukapewa siku 14 za kujiandaa ila siku hizo zimeisha Hela ya kujikimu hujapewa. Je unaweza subiri mpaka upate Hela ya salary au ? Maan eneo la kazi lipo mjini na gharama ya kuendesha maisha ni ngumu bila hela
 
Itabidi ukope ili uende hela ya kujikim wakat mwingine haitok mapema ninavyosikiaga lkn

Sent from my TECNO KH6 using JamiiForums mobile app
 
Hela ya kujikimu ifute kwanza kwenye kichwa chako japo utaipata ila itachelewa subiri tarehe 23 ulipwe salary
 
IT vita yetu haijaisha press botton wapambanaji kwenye huu uzi walambe asali asibaki hata mmoja
[emoji95][emoji95][emoji95].
Mzee IT mbona atasinzia kidogo maana mkeka wa tar 13 ,14 una nyomi la watu kama 700+ naona kama nyomi la masjala ya wazi kesho litakavyokuwa .

Mimi naona mkeka mwingine mpaka wiki ipite sina uhakika
 
Usiende kazini hadi mshahara utoke. Kama unaona wako strict sana nenda kaongee face to face na HR mwambie naomba ofisi inikopeshe sina nauli sina hela ya kupanga nyumba kama watashindwa basi omba ruhusa usubirie salary. Hao usiwaogope ni binadamu tu.
 
Nimekumbuka namna ambavyo nafasi 13 za Afisa Mambo ya Nje ziliajiri watu bila mambo kueleweka baadae zikatangazwa nyingine 18 nazo zikafutwa. Ndugu zangu kuna idara mambo hayaeleweki ukipata sehem shukuru Mungu
 
Hapo njaa Kali. Hakuna asiyependa mtori au supu ya utumbo ya moto na chapati kadhaa. Wewe ripoti anza kazi lakini notes zako zilizokufikisha hapo usitupe. Endelea kuongeza received
Sasa mtu unaenda halmashauri unategemea ukute watu wanakunywa supu kweli jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…