Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwako kipimo cha kufanya vizuri ni kipi katika hizi sahili mpaka inapelekea wengine kutokea database, tuambie hapo.
 
Kwako kipimo cha kufanya vizuri ni kipi katika hizi sahili mpaka inapelekea wengine kutokea database, tuambie hapo.
Kipimo Cha kufanya vizuri ni kupata kazi, hilo namba moja, kipimo cha kufanya vizuri zaidi ni kupata sehemu nzuri zaidi kuliko Halmashauri full stop

Ukiona mtu anaenda Taasisi na mwingine anaenda halmashauri wote wamefanya vizuri ila wamezidiana, alienda Taasisi kafanya vizuri zaidi haijarishi katokea Database au katokea frontline

Tatizo hamtaki kuamini kuwa mchakato wa kupokea mfanyakazi wa Taasisi na halmashauri uko tofauti, nikuulize wewe hujaona watu wanatoka kwenye placement Taasisi Fulani let's say mwezi wa 8 na kazi wanakuja kuanza mwezi 12?

Sasa Taasisi zingine zinaamua kukwepa lawama za waja, wanaamua watu wao wawekwe pending hadi pale mchakato utakapokuwa umekamilika ndio waitwe kazini, kwahiyo Kwa kipindi hicho chote watakuwa wapo Database ila well-known wanaenda wapi
 
Mkuu umeeleza kwa kina na kwa uyakinifu Sana.
Tatizo ni wenyewe utumishi ndiyo husema ukiona kwenye PDF jina la kwanza kuitwa kwenye kada ulifanyia usahili ujue huyo ndiye alifaulu kwa alana za juu kwenye Oral interview.
( Hivyo, ndiyo maana tunaona kwa maelezo yao Placement huwa Ina determine ufaulu wa oral interview).
 
Kipimo Cha kufanya vizuri ni kupata kazi, hilo namba moja, kipimo cha kufanya vizuri zaidi ni kupata sehemu nzuri zaidi kuliko Halmashauri full stop
Mtazamo wako ni tofauti na wanavyofanya kazi Utumishi.

Soma baadhi ya mistari toka matangazo ya kuita watu kazini.

"Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji
kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika
tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye
kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya
nafasi kupatikana.

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika
Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku
saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na
wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa
Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa
na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili
vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo
katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite
kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
 
"Kwa wale ambao majina yao hayapo
katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite
kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa"

Mkuu hebu tubishane kama wasomi basi, kwahiyo hayo maneno hapo ndio yanamaanisha waliokuwa Database wamefeli interview?

Mfano Kuna kazi zilikuwa zinahitaji watu 10, Ila placement ya Kwanza ikatoa watu 5, ya pili watu 4 naya Tatu ikatoa mtu 1 kukamilisha watu 10, je kuna placement yoyote ya mtindo huo imewahi kutoka bila hayo maneno ya kusema ambao hawajaona majina yao wajue hawakupata nafasi/hawakufaulu usahili?

Hayo maneno yapo ili kuondoa changamoto za watu kuwa na matumaini makubwa Sana ya kupata kazi, utumishi sio wajinga kwa sababu wanakuandaa kisaikolojia ili usiwe na matazamio makubwa kama wengi wetu tulivo humu, mtu anaacha kufanya Mambo mengine anakaa anasubiri placement

Hayo maneno yangekuwa yanamaanisha kilichoandikwa basi placement zingekuwa zinatoka mara 1 Tu na idadi kamili ya watu wanaohitajika, sasa iweje katika watu 40, waanze 15,kisha 10,kisha 7,kisha 8 alafu muda huo huo kila placement inayotoka mnaambiwa kama hujaona Jina lako ujue umefeli interview

Unakuwa umefeli vipi interview ilhali kazi ilihitaji watu 40 ila yameanza kutoka majina 15? Then next placement pamoja na kuambiwa ukiona Jina lako halipo ujue umefeli usahili ila unaona wengine tena, kwahiyo unamaanisha Utumishi wanawapa kazi watu waliofeli sasa au sio?

Tujitahidi tuwe tunashirikisha Akili zetu vizuri kwenye vitu vya simple logic kama hivi MwanzoMgumu2025
 
Wadau ushauri Kwa mtu aliye chelewa kuchukua barua utumishi na kuripoti kazini Kwa miezi minne anatakiwa afanyeje? Jina lilikua kwenye kanzidata na akachaguliwa kipindi kirefu sana baada ya kutokutokea kwenye mkeka wa kwanza
 
Wadau ushauri Kwa mtu aliye chelewa kuchukua barua utumishi na kuripoti kazini Kwa miezi minne anatakiwa afanyeje? Jina lilikua kwenye kanzidata na akachaguliwa kipindi kirefu sana baada ya kutokutokea kwenye mkeka wa kwanza
Barua watakua wamemtumia kwenye anuani aliyoweka, akachukue aende nayo kazini akawasikilize....kazi ua wanachelewa kuanza.
 
Oral niliifanya tu vizuri,na mpaka sasa status inasoma selected for oral interview both web na app, wasiwasi wangu ni kuwa isije ikawa kwa vile nimepata hii ya contract wakaninyima zile za permanent
huwezi pata ya permanent mpaka contract yako itakapokwisha. tayari wewe umejumuishwa kwa watu waliopata ajira kupitia utumishi pasipo kuzingatia aina ya ajira uliyopata.
 
Ulichoongea umekitoa wapi?
Naona majibu yangu hayakupi kile ulichotamani kukisikia, lakini huo ndiyo ukweli...watu wamekupangia kazi ufanye na wakati wanakupa kazi hiyo kuna watu waliachwa ukachaguliwa wewe, leo hii wakupangie tena kazi nyingine halafu mwajiri wako wa zamani akose mtu. Hebu kuwa muwazi hata ungekuwa wewe ungeweza kufanya kitu kama hicho?
 
Tumeshaona sana mtu akiitwa sehemu mbili tofauti kwa muda tofauti
 
Tumeshaona sana mtu akiitwa sehemu mbili tofauti kwa muda tofauti
Hayo yalikuwa makosa tu ya kimfumo, kitu kama hicho kwasasa hakipo au kimupungua kwa asilimia kubwa sana. wewe elewa tu hukutakiwa kwenda kuripoti kazini pale ulipopata placement za contract, lakini kama ulienda kuchukua barua na ukaripoti kazini hesabu maumivu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…