"Kwa wale ambao majina yao hayapo
katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite
kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa"
Mkuu hebu tubishane kama wasomi basi, kwahiyo hayo maneno hapo ndio yanamaanisha waliokuwa Database wamefeli interview?
Mfano Kuna kazi zilikuwa zinahitaji watu 10, Ila placement ya Kwanza ikatoa watu 5, ya pili watu 4 naya Tatu ikatoa mtu 1 kukamilisha watu 10, je kuna placement yoyote ya mtindo huo imewahi kutoka bila hayo maneno ya kusema ambao hawajaona majina yao wajue hawakupata nafasi/hawakufaulu usahili?
Hayo maneno yapo ili kuondoa changamoto za watu kuwa na matumaini makubwa Sana ya kupata kazi, utumishi sio wajinga kwa sababu wanakuandaa kisaikolojia ili usiwe na matazamio makubwa kama wengi wetu tulivo humu, mtu anaacha kufanya Mambo mengine anakaa anasubiri placement
Hayo maneno yangekuwa yanamaanisha kilichoandikwa basi placement zingekuwa zinatoka mara 1 Tu na idadi kamili ya watu wanaohitajika, sasa iweje katika watu 40, waanze 15,kisha 10,kisha 7,kisha 8 alafu muda huo huo kila placement inayotoka mnaambiwa kama hujaona Jina lako ujue umefeli interview
Unakuwa umefeli vipi interview ilhali kazi ilihitaji watu 40 ila yameanza kutoka majina 15? Then next placement pamoja na kuambiwa ukiona Jina lako halipo ujue umefeli usahili ila unaona wengine tena, kwahiyo unamaanisha Utumishi wanawapa kazi watu waliofeli sasa au sio?
Tujitahidi tuwe tunashirikisha Akili zetu vizuri kwenye vitu vya simple logic kama hivi
MwanzoMgumu2025