Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,474
- 125,866
Endelea kuwa na subira. Kama placement zilianza April mwishoni(hapo tuhesabu ni early May) muda wa data base utadumu hadi May/June mwanzoni mwaka huu. Kwa hiyo database yako bado ipo active sana.January 10/11 mwaka 2023 kama sikosei ni siku ambayo nilipata matumaini makubwa Sana baada ya kuufwatilia huu Uzi kimya kimya baada ya kumuona mwamba, mwamasishaji mkubwaa wa Uzi kuingia kwenye pipa la asali, hazikupita siku nyingi January 12 mwezi wa 1 mwaka 2023 na Mimi niliitwa kwenye interview kupitia shuhuda za wadau nilipata ujasiri maana nilishakata tamaa nikahudhuria iyo interview ilikuwa ni written, nikatoboa vizuri sana, February 15 tukaitwa oral placement zikaanza tokea anzia April mwishoni na sasa nakaribia kufikisha mwaka kama ni database inakaribia kuexpire, yote kwa yote jitihada ni muhimu sana, huu Uzi unamatumaini makubwa Sana kwa jobless maana ulinifanya na Mimi nijaribu tena jitihada zangu mpaka kutoboa oral interview, kikubwa tusikate tamaa tuzidishe jitihada Ipo siku na sisi tutatoa shuhuda, mapambano yaendelee
Muda ukifika utapata nafasi, nina imani oral uliifanya vizuri.
Kundi langu tuliloenda Oral kwa pamoja hadi sasa tushapata nafasi wote ingawa kwenye Oral tulikuwa tunapambania nafasi 1, ila wengine walikuja kuanza kuchomolewa kutoka data base.