Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mrejesho:

Kwakweli ni kwamba mimi kwa mara ya kwanza nilifika utumishi kwaajili ya written interview. Niseme tu nilifika Dodoma saa saba usiku kutokana na mazingira ya kusafiri kuwa magumu.Mara baada ya kufika sijuwa na sehemu ya kufikia,hivyo ilinilazimu nikeshe barabarani sehemu ambapo watu wapo muda wote.Asubuhi nilinunua maji nikanawa uso na kuchukua toyo mpaka UDOM.

Nilipofika nilihamaki uwingi wa watu! Nikasema Mungu hiki ni nini? Nikajisemea nimekuja kufanya nn huku? Nikiwa ninaonekana mshamba na upweke nisiye na hata rafiki wa kujadili naye chochote nikiwa nimesimama pembeni ya lecture theatre 1 kule college of business and education.

Baada ya muda walifika wasimamizi wakaanza kagua vyeti,nikafoleni nikaingia nikiwa na unyonge,ushamba,uchovu na usingizi mkubwa huku nikiwaza kuwa I am just trying.

Kweli paper ikaletwa,tukaelekezwa then tukafanya.Kiukweli ilikuwa NGUMUUUUUUUU! Ila inafanyika kwa wale wasomi na wafuatiliaji wazuri wa sera ya serikali katika utoaji wa mikopo kwa elimu ya juu.Ufanyaji wangu ulikuwa ni wa kujikongoja,huku nikihakikisha kila swali nagusa.

Nilijibu short and clear. Huku nikiwa nimekata tamaa. Ila kuna wanaume na wanawake haswaa waliomba hadi karatasi ya pili.Nilitoka na kuwahi stand nikapata chochote na kuanza safari ya kurudi kijijini kwetu nikiwa sina matumaini Yoyote.

Matokeo:

Leo nimeshikwa butwaa et nipo SELECTED FOR ORAL! Sikutegemea kabisa.Msimamo wangu ni kuwa nitarudi tena Dodoma kuwasikiliza maboss wakandaji live,nitakwenda KUJARIBU hiyo Oral.Sijawahi simama kwaajili ya Oral ila niwakute hukohuko hao wakandaji.Nikikosa basi,nitashukuru Mungu kwa kila kitu.

Kila lakher kwa woteeee mnaopigania huko,Mungu awafungulie njia.
Hongera
 
Mfano Kama mtu hana professional experience wala hakuwah kufanya intern ya fani aliyosomea, let say alimalizaga chuo akaendela na biashara zake tu. Alaf akafanya interview kwa mara ya kwanza akabahatika kufika mpaka oral! Hpo kweny kuelezea kuhusu professional experience anapaswa kusema nn?
Kwenye chuo lazima ulienda field dear, hiyo ndo internship
 
Oral interview tips:
1. Omba Mungu

2. Confidence, ukijibu swali jitahidi kujibu kwa utulivu na chukua muda kidogo kutafakari swali linataka nini kabla ya kujibu kwa pupa na kisha kuishia njiani na kutokujua jinsi ya kuendelea na kuonekana hujui kitu kumbe unajua!

3. Kujiandaa, hakiksha unasoma taarifa muhimu za taasisi unayoenda kufanyiwa usaili
unapojibu maswali hakikisha unaunganisha matarajio na maono ya taasisi na majibu yake

4. Usaili wa oral huwa mara nyingi huwa na maswali matano
swali la kwanza huwa ni tell us about yourself, mengine yataendana na kada/fani yako mengi huangalia general knowldege uliyo nayo.
swali hili la kwanza kila kada lazima uulizwe

ushauri: jibu kuanzia elimu yako, na nenda kwenye uzoefu wa kazi huku ukiainisha zile job descrption (jd) na uzoefu wako. Yaani onyesha uzoefu wako unavoendana na kazi unazotarajiwa kuzifanya
kisha elezea kitu/vitu vya ziada vinavokupa faida zaidi kwenye hio kazi.

5. Vaa vizuri, nguo zinazoendana kiofisi.

6. Wahi sehemu ya usaili nusu saa kabla

7. Beba nyaraka zako zote zinazohitajika.

8. Sema asante baada ya usaili kwa wasaili.

9. Unapofika sehemu ya usaili utakuta watu wengi, wasalimie unaowafahamu na usiowafahamu. Mtu akikuuliza kitu na unakijua usiwe mchoyo mueleweshe, mpe moyo. What goes around comes around. Mtakutana sehemu nyingine anaeza kuwa msaada kwako.

10. Ukimaliza usaili basi Omba Mungu tena na zaidi zaidi.
Kuna watu wana siti zao kwa Muumba zikiwasubiri kwa hamu.

Tuishi mkuu[emoji120]
 
Back
Top Bottom