Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Wakuu habarini...

Samahani kwa usumbufu Mimi mwalimu naomba kuelekezwa Kama address ya Kiingereza niliyoiandika ni sahihi

KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA, S. L. P. 2320, DODOMA.

Secretary
President's Office,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O.BOX 2320,
Dodoma.
 
Wakuu habarini...

Samahani kwa usumbufu Mimi mwalimu naomba kuelekezwa Kama address ya Kiingereza niliyoiandika ni sahihi

KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA, S. L. P. 2320, DODOMA.

Secretary
President's Office,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O.BOX 2320,
Dodoma.
Iko sahihi kikubwa usisahau kuisign iyo barua
 
Mwaka jana mwezi wa sita ilikuwa interview yangu ya kwanza kufanya nilimaliza chuo 2022.Kwa bahati nzuri Mungu akanisaidia nikaingia oral kwa mara ya kwanza.
Kimbembe ikawa ni kusubiria placement ...kwa kweli nilikuwa na kiherehere sana😅😅 ikawa kila siku nikulalamikia placement kwa nini hawatoi majina,nikaanza ku imagine siku nikiwa kwenye gari naenda kuchukua barua(ikumbukwe ni interview ya kwanza😂😂) basi nikawa moto na kila mtu home akawa ananipa matumaini ananiaminisha kwamba lazima utapata hii nafasi usihofu😅 nami nikaanza kujipanga kuanza kazi kama vile baba yangu ndiye anaeajiri watu kwamba mimi kupata ni uhakika...

Basi Mungu alivyo mwema mwezi wa 8 placement zikatoka kuangalia!!!.... too bad!!! sikuwemo nikahisi moyo kuvunjika sana maana expectation niliyokuwa nayo ilikuwa kubwa mno nikajipa moyo labda huenda ntapata kupitia database...baadae majina ya database yakawa yanatoka kila jina simo nikaanza kujikatia tamaa🤦🤦...baada ya Muda wakaacha kutoa majina kwenye database ya kada yetu kwa muda mrefu hapo ndo nikajua kabisa kuwa nilishakosa.

Basi nikawa nimekata tamaa na interview (japo nimefanya moja nilikata tamaa kulingana na maisha na gharama za kufanya interview dodoma) nikawa nimeridhia rasimi maisha ya kuwa mwanakijiji😅nikapoteza matumaini ikafika hatua mpaka nikaamua ku logout humu jf ili nisipost wala kucomment chochote.

Lakini Mungu alivyo wa ajabu jana pdf ya tarehe 20 nimeliona jina langu kwenye pdf kama utani tu yani😅😅😅(nina furaha kubwa sana na namshukuru Mungu)
Nilichojifunza ni kwamba kinachofanya maumivu ya kukosa jina lako kuwa makubwa ni kuwa na EXPECTATION KUBWA za kuamini kwamba utapata basi ukikosa unajikuta unaumia sana na kujiuliza maswali mengi.
...Niendelee kuwatia moyo ambao bado hamjafikiwa SIKU YENU ITAFIKA TUWEKE MATUMAINI KWA MUNGU NA KUPUNGUZA EXPECTATIONS TUTAFIKIWA TU🙏🙏
 
Waoga hao....waache wajisahau tu
Uzuri nimefanya interview mbili za utumishi moja nilikanda moja nilitoboa hadi oral.

Nimejifunza vingi sana.

Ila kwa uyakinifu siruhusu watu wa afya na walimu kukandwa Nina sababu 10 siku nikitulia nitatoa sababu.

All in all mm msakanyoka mwenzenu kuna pdf naendelea kuzfukuzia ila majobless tuna makasiriko jamani
 
Lazima wakandwe, watake wasitake [emoji23]
Ila mkuu mbaga jobless wanamakasiriko.

Juzi wakina mwifa wametuambia tupambane tuingie oral.

Leo mm nimeweka imani kwamba ninaweza kuitwa kazi kwa sababu nilifanya oral.
Ee mara kuna mtu ananiuliza una uhakika gani kama uko database.

Sasa nini maana ha kuhamasishana kufika oral na tukifika oral iweje wengine wakasirike.
 
Back
Top Bottom