Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Habari wakuu,,
Naomba msaada katika hili, sijawahi udhuria saili yoyote ila mwezi huu nategemea kuhudhuria saili kadhaa. Ipo hivi majina yangu kwenye vyeti vya kielimu yapo matatu ila jina la kati kati ni initial lakini majina ya kwenye NIDA na cheti cha kuzaliwa yanasoma yote matatu full
Mfano: vyeti vya shule Abdul J. Bakuri
NIDA: Abdul Juma Bakuri
Cha kuzaliwa: Abdul Juma Bakuri

Je,? siku ya usaili haiwezi niletea shida??
Ahsanten🙏
 
Hivi barua ya utambulisho ya mwezi wa pili ambayo ilitumika kwenye usaili unaweza kwenda nayo tena mwezi wa nane kwenye usaili mwingine au mpaka utafute nyingine ya mwezi wa nane

Nadhani inafaa. Maana kama serikali ya mtaa wamekutambua mwezi wa pili, haina maana ikifika mwezi wa nane utakua sio mkazi wa hapo. Nafahamu utambulisho wa SM unatumika in lieu ya kitambulisho cha taifa.
 
Ok Asante sana 🙏
 
Hiyo J inabidi uithibitishe kwa Kiapo kuwa ndio imesimama badala ya Juma.

Muone Mwanasheria akupe muongozo wa kiapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…