Hivi usaili wa online huwa unafanyikaje wakuu? Binafsi sijawahi Kufanya online interview.
Kwa taarifa ya jinsi hii system ilivyo ni kuwa, written interview (online) ni multiple questions, maswali 40 (Kwa maana Hadi Sasa waliokwisha Fanya Kwa kada mbalimbali), ni mfumo wa ku click jibu sahihi wewe na mouse yako tu. Huruhusiwi kubonyeza popote pale nje ya sura ya mtihani baada ya kuanza huo mtihani yaani ni ww na mouse yako ya kuchagua majibu.
Kwenye usaili Kuna maelekezo utapewa maana Bado ni mfumo mgeni lakini Kwa ufupi ni mfumo rafiki Kwa yeyote anaweza kutumia.
MAMBO YA KUZINGATIA.
Hakikisha ile email na password zako unazotumia kuingilia PSRS au huko ajira portal hauzisahau, kwasababu utazitumia hizo hizo kuingia kwenye huo mfumo wa usaili utakaokufanya ufanye hiyo written interview.
Usibonyeze vitu hovyo na kama huna hakika muite msimamizi akuelekeze. Usifungue tab mpya Wala kubonyeza bonyeza nje ya sura ya mtihani wako mbele ya kompyuta yako.
Muda wa mtihani ni mchache sana, ni dakika 50 tu au 40 (Kwa ambao tayari washafanya Hadi Sasa) hivyo Kila swali ni dakika moja na ushee.
Ndani ya lisaa kasoro ushamaliza na kumbuka usisahau kubonyeza "SUBMIT" mwisho kabisa baada ya kumaliza lakini hata usipobonyeza muda ukiisha inajisubmit automatically, pale juu kulia kwenye screen ya kompyuta yako Kuna muda una count, dakika na sekunde ndiyo zinahesabu tu pale juu, hivyo nenda na muda...vile vile unaweza kuanza na swali lolote lile na kurudia (kujibu) Yale mengine uliyoyaacha ilimradi uko ndani ya muda, kumbuka hata kama hujamaliza muda ukiisha pale juu jua ndo basi tena inajisubmit.
La mwisho kumbuka kusoma vizuri, usipite hvhv maana multiple questions hizo ziko very tricky hasa ukiwa hujasoma, soma virahisi, vya kati na vile vigumu...hii ni tofauti na ile ya mwanzo unaweza kukutana na familiar questions ila hii ya Sasa ni ngumu.
Mwisho ni kwamba, matokeo yako utayapata siku ile ile (kwenye akaunti ya ajira portal)hivyo aidha unaenda Dom au unaendelea na mambo yako.
Hii ni tip kidogo naamini itakupa mwanga kidogo.