Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

The meaning of wanaume tumeumbwa mateso🀣🀣🀣
 
Yaani ukichanganya kigezo na GPA na kusoma masters na kuendelea utawapata wachache sana.


Iko hivi mwenye GPA kubwa hana uwezo wa kusoma Hadi master na kuendelea na mwenye uwezo wa kusoma postgraduate hana GPA kubwa. Mambo mvuruganoo😜😜
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Vurugu tupu duniani ni mwendo wa ngiri tu
 
Written yangu ya kwanza tulikutana na watu 3 ambao wanajitolea kwa mwajiri aliyetangaza hizo nafasi.

Mmoja ambaye namjua(wengine nilikuwa siwafahamu ila niliambiwa na watu waliokuwa wanawafahamu) huwa ananihudumia pindi nikiwa na shida katika ofisi hiyo.

Kuja siku alikataa nyaraka zangu kisa nimetoa kopi kwenye kopi yenye muhuri wa wakili, nilimind ila hakunisikiliza/hakunielewa/hakukibali.

Kuna mfanyakazi mwingine nilikuwa nishajuaana naye(kwa sura ila sio majina na nilizoeana naye), nikaenda kumueleza jinsi nyaraka zangu zilivyokataliwa, baada ya kunisikiliza akakubali na kuzipokea.

Huyu aliyezikataa nilidhani ni muajiriwa pale.

Siku ya written nilipotinga pale CIVE tukiwa tumekaa nje kusubiri utaratibu, nikamuona akaja nikadhani amekuja kusimamia mtihani(sikujua kama PSRS ndio jukumu lao hilo), wakati tunaendelea kusubiri ndipo nikagundua na yeye amekuja kwenye usahili.

Tulipiga written, tukakandwa wote(mimi na yeye), ndipo nikaamini kujitolea hiyo sio tiketi ya kufaulu UTUMISHI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…