Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

😂😂😂😂Yani ukishaona mwanamke mpo nae ujue hapo hamna chenu nakumbuka oral moja tuiingiaga watu 11 kati yetu alikuepo mdada mmoja nandiye aliyepata kazi sema kwa nilivyopigaga nae story wala hakuwa na uwezo mkubwa maana Kuna maswali aliniulizaga afu niyakawaida tu ambayo yeye alikuwa hayaelewi
The meaning of wanaume tumeumbwa mateso🤣🤣🤣
 
Yaani ukichanganya kigezo na GPA na kusoma masters na kuendelea utawapata wachache sana.


Iko hivi mwenye GPA kubwa hana uwezo wa kusoma Hadi master na kuendelea na mwenye uwezo wa kusoma postgraduate hana GPA kubwa. Mambo mvuruganoo😜😜
😂😂😂😂😂Vurugu tupu duniani ni mwendo wa ngiri tu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Tatizo wanaojitoleaga wanakuaga na dhalau sana sisi tuliendaga kupiga interview na wale wanaojitolea kwenye written sasa tukakariri namba zao majibu kuja hawakupita kwenda oral sema wanakuaga na dhalau sana yani hata ukimuuliza hiki kinaendaje Hataki kusema mamaaaae sana
Written yangu ya kwanza tulikutana na watu 3 ambao wanajitolea kwa mwajiri aliyetangaza hizo nafasi.

Mmoja ambaye namjua(wengine nilikuwa siwafahamu ila niliambiwa na watu waliokuwa wanawafahamu) huwa ananihudumia pindi nikiwa na shida katika ofisi hiyo.

Kuja siku alikataa nyaraka zangu kisa nimetoa kopi kwenye kopi yenye muhuri wa wakili, nilimind ila hakunisikiliza/hakunielewa/hakukibali.

Kuna mfanyakazi mwingine nilikuwa nishajuaana naye(kwa sura ila sio majina na nilizoeana naye), nikaenda kumueleza jinsi nyaraka zangu zilivyokataliwa, baada ya kunisikiliza akakubali na kuzipokea.

Huyu aliyezikataa nilidhani ni muajiriwa pale.

Siku ya written nilipotinga pale CIVE tukiwa tumekaa nje kusubiri utaratibu, nikamuona akaja nikadhani amekuja kusimamia mtihani(sikujua kama PSRS ndio jukumu lao hilo), wakati tunaendelea kusubiri ndipo nikagundua na yeye amekuja kwenye usahili.

Tulipiga written, tukakandwa wote(mimi na yeye), ndipo nikaamini kujitolea hiyo sio tiketi ya kufaulu UTUMISHI.
 
Back
Top Bottom