Habari zenu wakuu, nlkua naomba nisikie mawazo yenu juu ya hili, japo ni nje kidogo ya mada wa uzi huu.
Nipo nafanya kazi na kampuni moja ivi, lkn bado naendelea pia kutafuta na sehem zingine ili kupata atleast sehemu nzuri zaidi.
Nikabahatika kuitwa na kampuni ingne for interview, nikaenda nikafanya, na wakanipigia tena simu kesho yake kuwa nimepata kazi na niende kwa ajili ya taratibu zingne.
Ikabidi niombe ruhusa oficin ya dharula niende, nilivyofika waliniambia vitu ambavyo itanibid nivipeleke kwa ajili ya kuopen file na moja ya ivyo vitu ni barua ya kuacha kazi sehem ambayo nipo sasa ivi. Nikaomba atleast wanionyeshe mkataba nione salary yao ikoje ila waligoma kabisa, nilijaribu kila mbinu atleast niweze kujua mshahara wao ukoje ikashindikana, na hawataki kunionyesha mkataba mpaka nipeleke ivyo vitu plus iyo barua ya kuacha kazi. Na ni kampuni kubwa tu hapa nchini.
Hii imekaaje wakuu?! Maana naogopa kurisk hapa nilipo sasa hivi, then nikafika kule nikakutana na mambo meusi.
Ntashukuru kwa mawazo yenu.