Bora kuwai ndugu zangu, mie nishawai kukosa usaili kwa kuleta mazoea pale CIVE...usaili ulikuwa saa 1 kamili nikachukulia poa kutokana na idadi ya watu tulioitwa zaidi ya buku nikajua ukaguzi hadi kuanza itakuwa saa mbili ...daaah kumbe siku hiyo wakandaji waliwai mapema sana saa 12 tu walishatia timu pale machinjioni CIVE na mbaya zaidi wasailiwa walifika wachache tu kati ya watu 1000+ waliofika hata 50. So mie nilipofika pale ndio jamaa bado kidogo tu watoke pia sikuwa peke angu niliuechelewa tulikuwa wengi tu. So mazoea ni mabaya siku hizi mapema tu nishafika. Kilichoniumiza zaidi siku hiyo niliwai kuamka pale lodge nilipofikia ila kwakua usaili wa bunge tuliambiwa saa 3 Asubuhi ila tulifanya saa 10 kasoro jioni nikajua mambo ni yaleyale but hiyo cku ikawa tofauti