Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ni ASA, mkuu naomba nisitaje post yake kwa privacy zaidi.

Nadhani yupo humu, kuna mtu kila nikizisoma komenti zake, nahisi atakuwa ni yeye, wanafanana sana hoja zao na uandishi.
Sawa sawa kiongozi nafikiri awe anaulizia kwa wengine jinsi yakujiandaa kusoma kabla na jinsi yakujibu mitihani ile ,inaweza kumsaidia wakati ujao lakini asikate tamaa
 
Haya mambo ya written ni Bahati sijui, jumamosi kilichotokea daah..
Ngoja tusubiri matokeo

Nakuunga mkono sana Mkuu, yaani mdogo wangu namuamini sana, na kweli kuna moja alitoka akasema imembana sana ila nyingine mara nyingi anasema zimekuja aliposoma ila shida ni matokeo yake huja mabaya.

Nadhani haya masomo ya kuelezea nayo yana shida kuliko masomo ya facts kwa sababu yanampa msahishaji mamlaka ya kuamua alama.

Hata hivyo naamini siku yake haijafika, endapo ikifika haitokuwa na kizuizi zaidi ya kufanikiwa kiulaini.
 
Shida inaweza kuwa jinsi anavyojibu maswali au anaweza kuwa alilielewa swali vibaya
Kwamfano unaweza ulizwa
Describe land forms of geomophic process
Au Describe features due to geomophic process
Hayo maswali ukiyaangalia ni kama yanafanana lakini yapo tofauti kwahiyo kwenye zile pepa ukiyumba kulielewa swali yani ujue marks 25 zote hazipo tena
 
Hizi paper mara nyingi zinahitaji mambo makuu kama matano.

1. Kuelewa maswali
2. Kuandika kwa kifupi, usiweke mambo mengi sana.
3. Speed ya kuandika iwe kubwa, maana dakika 40 ni chache sana ukishaingia mule. Andika kwa speed ya jet. Watu huwa hawamalizi maswali kwa kuandika polepole.
4. Maandalizi kabla ya paper. Jiandae na usome vizuri.
5. Kama unaamini ktk Mungu, omba.
 
Matokeo yanakuja mabaya kwamba huwa anatapata marks ngapi au pengine hajawahi kufikisha marks ngapi
 
Shida inayowamaliza wengi ni kutolielewa swali na kushindwa kumaliza maswali maana watu wengi hujibu kama gazeti
 
Namimi mdogo wangu wamemnyoosha kwa mara nyingine tena. Kwa sasa ameshafanya saili tatu mfululizo na zote hana chake.

Ngoja tusubiri zinazokuja.
Aisee tuwaombee wadogo zetu na majobless wote wapate mrija wa asali...mimi mdogo wangu tangu 2019 anafanyaga interview ila ndio hivyo bahati haiwi upande wake ....namuonea huruma na kama familia tunamsapot ....ngoja tusubiri maana juzi kati kafanya interview hizi za LGA NA MDA kama auditor amefanya oral na nilikuja kumuulizia hints humu za kujibu oral nashukuru wadau walinijibu nikampa nondo hope this time mambo yatakuwa mazuri upande wake ...nitaleta mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…