Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Sasa utumishi tatizo nini miezi mitatu watu tangu mwezi wa tano hadi leo wa tisa na bado saili zinaendelea
 
Sasa utumishi tatizo nini miezi mitatu watu tangu mwezi wa tano hadi leo wa tisa na bado saili zinaendelea
Sababu zinaweza zikawa nyingi ikiwemo.
-Ukosefu wa nguvu kazi(watumishi)
-Ukosefu wa venue pindi vyuo vikiwa vinaendelea na masomo
-Kukosa support kutoka kwenye taasisi husika zlizoomba kutafutiwa wafanyakazi, hili la support vyuo wameweza kama tunavyoona wanaendesha saili zao kwa kushirikiana na PSRS.
 
Mambo yamebadilika siku hizi
 
Mwifwa mbona ,Kama uko kwenye system Mzee,
Unajibu maswali in depth, informations za ndani ndani kabisa.
Ila endelea kutupa madini, hatuna namna
Laiti mzee wa Aliyeondoka asingebadili mfumo wa ajira nisingehangaika kuutafuta mrija wa Asali namna hii, ningeingia moja kwa moja baada ya kusajiliwa na kupata leseni ya kazi kutoka kwenye baraza langu la Kitaaluma.

Ingawa mtaani tunabangaiza bangaiza vijisenti vya kusogeza siku ila havina security, nchi yetu security ya vijisenti ni muhimu sana, ambapo kwa uhakika wa asilimia kubwa tunaipata huku Gavo.

Ni bora upate(ujira) kidogo palipo na uhakika wa kukipata kuliko na kupata kikubwa pasipo na uhakika wa kukipata, yaani hicho kikubwa ukikipata leo halafu kukipata tena hadi uzidishe maombi usiku na mchana. Ni taabu.

Ingawa hili ni mtazamo ya watu mbali mbali, na hatuwezi kufanana mitazamo kwa hiyo kila mtu anaamua kuchagua wapi pa kushika.

Tuendelee kupambania mrija wa Asali popote tunapoona panafaa
 
Hahahahaa, bado nawaza jinsi nilivyokandwa zile written 2.

Mtu wangu wa karibu aliyefika oral hata bado sijamuuliza jinsi oral ilivyofanyika, nimebaki najitathimini ivi kweli nimekuwa mdebwedo kiasi hiki.

Ahsante kwa kunikumbusha hilo.
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†pole babe,utumishi hawatabiriki
 
Sahihi basi wamekuwa hawalazi vipolo mda mrefu mambo yanazidi kuwa mengi mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…