Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Aisee hii kitu inaumiza, unakuta ni watu ulikuwa unajiandaa nao na wengine unawaona kabisa hawakuwa serious lakini ndio hivyo wamepita na wewe umebaki.

Muda wako utafika Mkuu, endelea na mapambano.
Kuna madereva wa tra wataaenda kukandwa hivi karibuni ,katika interview matata moja wapo ni za udereva ,kukandwa kupo pale pale haijalishi dereva mkongwe au siyo mkongwe .

Kunaenda kufanyika written sehem mbalimbali mikoani ,ikiwemo dar ,dom,mbeya mwanza na hata Zanzibar ,baada ya pale wote wanakutana dar kwa ajiri ya kukandwa kwenye test

Nachotaka kusema ,kama haujawahi kufanya test yoyote pale veta Chang'ombe umakini unahitajika sana.
Gari zao zimechokonolewa sana,kuna hiyo tata ya wanafunzi huwa inatumika kwa test. Gia liva yake ilisha chokonolewa ,gia ni za kutafuta,pili hiyo gari haihitaji mwendo sana,tembea 40-50km/h .Ukizidisha hapo gari inaanza kuyumba.

Kuna leyland pale na kuna scania 94 ,hizi zote hutumika ,pale hupewi land cruiser.hivyo umakini unahitajika likija zoezi la test .

Wengi huwa zinawashinda ,hasa hiyo Tata ni ya kuiangalia sana,bora uende kwenye 94 ila pia leyland sishauri labda kama ulishaendesha hapo awali.Ni hayo tu wazee wa kukandwa
 
Hiv Ile hbr ya waziri wa elimu prof. Mkenda kusema ajira za wakufunzi vyuoni hawataangalia GPA ,tu hvyo lazima mtu apimwe uwezo wake kweny presentation na Q&A ,
Hizi ajira zitakuwa hata wenye GPA ya lower class atapata nafasi as long as anao uwezo ,,sjaelewa???
 
waendelee tu kuangalia GPA mana wengine ndo zinazotubeba[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nadhani alikua anamaana kwamba hawachukuliwi kwa GPA tu kama zamani wanapitia mikando yote miwili. Hivyo, GPA ni criteria ya kwanza ya kuchuja na itaendelea kubaki pale pale.
 
Hongera sana.....
 
Ila haujajibu swali langu
Kwa sababu ana shida kama yangu, ngoja nimsaidie kujibu.huko secondary walimu huwa ni wazembe sana mfano mtoto anaitwa Samia Suluhu Hangaya.wao wanamsajili kama samia s hangaya,necta nao wanapelekewa same data,so ukifika chuo watadai cheti chako cha kuzaliwa na data zako watazozitumia kuandaa cheti chako na transcript ni za kwenye cheti cha kuzaliwa na kitambulicho cha nida..Anyway mimi nashukuru utumushi hawajawahi kunizuia kufanya paper coz ya huo mkanganyiko.
 
Hongera sanaa mkuu....Kila la kheri kwako

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu kwema naomba kuuliza mimi nimeitwa kwenye written examination ya tarehe 18 ila nimepangiwa mbeya wakati kwa sasa nipo Mwanza hivi hamna namna naweza fanya ili nifanyie kituo cha Mwanza huku huku
 

Mkuu, habari ni njema. Naamini zitakuwepo shuhuda za ambao hawajawahi kuzuiliwa na ambao wamewahi kuzuiliwa.

Kwanini ufanye bahati nasibu kwa ajira zenyewe hizi zisizotabirika saa wala dakika ya kuzipata?

Hebu tafuta affidavit ili ufanye maandalizi kwa kujiamini na hata muda wa ukaguzi wanaokagua wakose sababu ya kukukwamisha.
 
Wakuu kwema naomba kuuliza mimi nimeitwa kwenye written examination ya tarehe 18 ila nimepangiwa mbeya wakati kwa sasa nipo Mwanza hivi hamna namna naweza fanya ili nifanyie kituo cha Mwanza huku huku
Fuata maelekezo ya ofisi ya utumishi, hicho pia ni kigezo cha mchujo.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 

Duh! Mkuu kwa niaba ya wengine, asante sana kwa kutupa dodoso zuri.
 
Njoo nikuandalie affidavit chaap, halafu husirudi humu kushuhudia Prok ni nan[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…