Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?


Hahahaha! Sawa Mkuu. Wanasema kinachosababisha urafiki ni kuwe na mfanano unaowakutanisha. Japo wengine sababu zilizotuleta kwenye huu uzi ni tofauti lakini asilimia kubwa ni watafuta ajira.

Sasa inshu ni mtu akishapata ajira, automatically anakosa chakumuunganisha na wanaopatikana kwenye huu uzi.

Wakati yeye atahitaji watu wa kujadili nao kwanini Serikali imesimamisha kupandisha madaraja ya watumishi wa Umma, akiingia humu atakuta watu wanabishana kuhusu status baada ya Oral au wanamlaumu mtu anayepandisha Pdf kwenye website ya utumishi kwanini hapandishi siku za Jumanne kama alivyowazoesha.

Baada ya muda ataona michosho na kuingia mitini kwenye nyuzi nyingine.
 
Naombeni mnipokee msaka mrijaa wa asali mwenzenu. Nimekuwa nikiufatilia kwa muda na nimejifunza vingi sana. Mpaka sasa Nishafanya saili kama 6 na zote nimekandwa.

Karibu sana Mkuu. Nakutabiria Oral yako yakwanza itakupa na kazi moja kwa moja.

Usichoke, endelea kupambana huku ukijifunza kupitia mapito yako.
 
Au wengine watahamia kwenye uzi wa magari makali akajichagulie subaru huko[emoji3][emoji3]
 
Au wengine watahamia kwenye uzi wa magari makali akajichagulie subaru huko[emoji3][emoji3]

Hahahaha! Niliona watu humu wameshaanza kushauriana gari gani inafaa kuwateka wadada bila kujali itahitaji service ya kiasi gani au inakunywa mafuta kiasi gani.

meck pro, Ahmet na wizy sipati picha mishahara yao ya miezi mitatu ya kwanza wataifanyia nini, inawezekana wakafanya starehe za kutosha kuuaga ujobless.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…