Kuna Mwl wangu fulani nilipokuwa Form 2 aliwahi kusema "Kufaulu mtihani sio kufaulu maisha", kwa kipindi hicho hiyo kauli sikuweza kuielewa ila nilikuja kuielewa tayari nikiwa nishapata elimu ngazi ya degree.
Mimi ni miongoni mwa Mwanafunzi pekee niliyebahatika kuchaguliwa shule ya Bweni kutoka kijijini kwetu, wengine walitupwa shule ya kata, wengine wakatupwa kitaa(hawakufaulu almaarufu kuPASS kwa enzi hizo).
Cha ajabu sasa ambao hawakuPASS wengi wao ndio wakawa wa kwanza kutoboa life.
Tuliong'ang'ania njia ya kalamu kama njia ya kutoboa ndio tumebaki wa mwisho kwenye hizi races za kutoboa, huku tunabaki kutojua kumbe tulipoteza sana muda ingawa tukipata mirija ya Asali tutaweza kufanya come back ya kibabe kama Mbappe juzi.
Takwimu zinaonesha kuwa, darasa letu Primary tuliofanikiwa kupata degree moja kwa moja ni 2 tu (Mimi na meingine alisoma Ualimu). Wote na degree zetu bado tunapambana kusaka mirija ya Asali, yule wa Education ajira za moja kwa moja tunajua Mwendazake alizisimamisha ,juzi kwenye Interview za Bunge niliona kaitwa kwenye mkando(sijui kama alienda au la).
Kwa kifupi tuliokuwa wa kwanza zamani, sasa tumekuwa wa mwisho. Life halina formula.
Sifikirii kurudi shule, hii degree 1 inanitosha, sasa naisaka degree ya mtaani kwa mgongo wa mrija wa Asali.