Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hyo ratio ni nzuri kwa harakati za kubaki database Ila kwenye kinyang'anyiro cha kazi officially ina kaugumu kutuboa Ikiwa upo na watu nondo kukuliko
 
Nakazia kuhusu ratio, yaani Selected for Oral.
 
Hyo ratio ni nzuri kwa harakati za kubaki database Ila kwenye kinyang'anyiro cha kazi officially ina kaugumu kutuboa Ikiwa upo na watu nondo kukuliko
Kweli mkuu, ila ukishafika oral, hesabu mnaanza upya tena.

Yeyote anaweza kutoboa kwenye hii stage.
 
Basi kumbe ukiona ratio imezidi hapo ni kukaza tu ili ufaulu na ubaki kanzidata maana ni uhakika.. halafu utam wa kanzidata unakuja pale unapoona umepangiwa taasisi ya maana kushinda wale wa mwanzo
A
Ila tuziweke pembeni taasisi za maana kama BOT.

Hahahahaa
 
Basi kumbe ukiona ratio imezidi hapo ni kukaza tu ili ufaulu na ubaki kanzidata maana ni uhakika.. halafu utam wa kanzidata unakuja pale unapoona umepangiwa taasisi ya maana kushinda wale wa mwanzo
A

Ni kweli sana Mkuu, japo kwa kuongezea nadhani raha ya kanzi data itakuwepo pia kama nafasi uliyoomba inaweza kupatikana kirahisi kwenye taasisi nyingine.

Kuna baadhi ya nafasi kulingana na alichosomea mtu, hata akikaa kwenye kanzi data ni mpaka taasisi hiyo hiyo au inayofanana na hiyo ipate tena nafasi. Hapo sasa ndio changamoto.

Nadhani miongoni mwa maboresho wangefanya mtu akishaingia kwenye kanzi data, sifa zinazoangaliwa iwe ni vyeti vyake vinamruhusu kupangiwa kazi gani na sio lazima iwe ni nafasi kama ile aliyoomba ikamfikosha Oral.


Ndugu mchambuzi na mwanasheria wetu wa thread na Jf kiujumla, uliyejikita kwenye masuala ya psrs Mwifwa ukipata nafasi naomba kwa niaba ya wengine utupe somo kuhusu kanzi data kwa vigezo vya psrs.
 
Ukifanya oral ukikaa kanzi data unapangiwa kazi yoyote ambayo taaluma yako unaruhusiwa, unaweza ukafanya oral ya wakili wa SERIKALINI ii unapangiwa baadaye Kama afisa tarafa ii
 
Pia utumishi upokea vibali vya kazi wakati saili zinaendelea, hivyo kanzidata hujaa watu wengine kwa ajili ya vibali vipya vilivyoukuta mchakato unaendelea kwa wataalam walewale
 
Hahahahaaah! Asante mwanasheria wetu wa uzi. Sikuwa najua kama hata kanzi data nayo huwa inakuwa na uhitaji.
Ni lazima iwe na uhitaji coz mara zote hawwezi kutangaza kazi na kupitisha saili hizi saili zinamatumizi yake ya pesa pia.. unaweza Kuta Halmashauri Fulani inauhitaji wa nafasi 1 hapa lazima wanyofoe mtu kutoka database
 
Kuna kanzidata za aina tatu:
1. Za wahitimu wa Vyuo na Wataalam
2. Za waliofaulu usaili
3. Za waliopangiwa vituo vya kazi.

Najikita kwenye Kanzi data ya waliofaulu usaili ambayo imezungumziwa kwenye kanuni namba 22.

Imelezewa kuwa orodha ya waliofaulu usahili mahojiano na hawakuweza kupata nafasi itatunzwa kwa matumizi ya baadae(1), itatumika kujaza nafasi wazi kulingana na mahitaji ya waajiri(2), endapo hii orodha itakuwa imeisha baada ya watu wote kupangiwa vituo vya kazi au waliopo kanzi data watakuwa hawana sifa au utaalamu anaouhitaji mwajiri, nafasi za ajira zitatangazwa(3),

Kulingana na hivyo vipengele vya kanuni inaonesha kuwa sifa au utaalamu wa mtu aliyepo kanzi data ndio utamuwezesha kupangiwa kituo endapo nafasi yenye kuhitaji sifa au utaalamu alionao itapatikana, hapa sasa ndio pale tunapoona watu wanapangiwa vituo kwenye taasisi tofauti tofauti ambazo hawakuzifanyia usahili.

Kuhusu kuangalia suala la qualifications za vyeti kama unavyotaka hapa mimi naona hili lipo ndani ya sifa au utaalamu uliotajwa kwenye kanuni hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…