Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ok.. taasisi tunazozitarajia ni November kama ifuatavyo:-HESLB,MDS' & LGA's hapa Kuna na wale wanasheria pia, OUT, SUA(Non teaching).
ASA, TARI, WIZARA YA KILIMO (TUTORS)- hizi zilifanyila December mwanzoni kabisa
Tabiri ipi itaanza Hapo๐Ÿ’ฅ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Finally I made it!

Kutana na Mwifwa- From three times defeat to Champion

Hii ndio ilikuwa safari yangu ya kusaka mrija wa Asali.

Mwaka 2021, safari hii ilishika kasi kwa kuapply mara 8( Sekta binafsi, Wizarani na Tamisemi). Kote niliangukia pua, Sekta binafsi sikubahatika hata kuitwa kwa usahili.

Mwaka 2022, kasi ikaendelea kushika kasi nilipoapply Wizarani na Tamisemi kabla ya kutimkia PSRS, mara hii niliangukia pua pia Wizarani na Tamisemi.

PSRS nilifanya application 5, 4 nikawa shortlisted, moja sikuwa shortlist kwa sababu isiyokuwa ya msingi maana hiyo sababu wangeizingatia nisingekuwa shortlist zile zingine 4.

Kwenye shortlist 4, tatu nikakandwa mfululizo hadi nikakata tamaa, ila wadau wa humu wakanipa moyo na nikapata nguvu ya kwenda kupambana.

Baada ya kwenda kwenye battle nikaingia oral kimasihara. The rest is history, what a joyful in my life history, my eyes are filled with joyful tears.

Join me in celebrating this remarkable history!!
Hongera sana kaka, hakika tumefurahi aisee... Umetupa moyo wengi hatimae na wewe unaenda kulamba asali hakika ni furaha ilioje
 
K
Habari za leo Wakuu.
Jana niliahidi kuleta mrejesho.
Nilifanya written Interview nane ,saba zote sikufika hata oral zote nilikuwa napata namba za viatu , yanane nikafika oral na ndo hii niliyopata placement.


Nilingia kwenye chumba cha wakandaji nikiwa nimevaa kadeti, shati na koti langu vizuri kabisa. Nilipoingia tu ndani nikawasalimia wakandaji wakaitikia then mmoja akasema karibu kiti.




Nilitumia muda mfupi sana nimetoka wadau wanashangaa mbona mapema sana nadhani walijua nimefukuzwa mle ndani๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Baada ya hapo nilijiona mjinga sana maana nimeshindwa kujibu swali moja. Hamu ya kula ilikata kabisa niliona kama nimepoteza nafasi lakin Mungu ndo alijua.
Nimejifunza ili ufanikiwe lazima upite mambo magumu( Rejea wimbo wa Christina Shusho-Dhahabu)

1. Usikate tamaa jipe moyo ipo siku utatoboa bahati huwapata wale wanaojaribu.
2. Ukiitwa kwenye usaili fanya maandalizi haswa. Piga msuli yatima haswa pitia job descriptions zifuatilie moja baada ya nyingine. Saili nyingi za nyuma nilikuwa sijindai vizuri pia nilikuwa sifuatili trends za maswali. Unakuta unasoma research kumbe wameshaacha kutoa research.
3. Omba Mungu yeye ndo anajua ni lini atakupa.
4. Usibanduke kwenye huu Uzi. Jamii forums ni kila kitu imagine nimeanza kufuatilia huu uzi mwezi wa 10 nikapata hints kibao nikafufua matumani , mwezi wa 10 huo huo nikatoboa oral kwa mara ya kwanza. Hata uwe kipanga au kenge namna gani bila kujua trends na namna ya kujibu maswali kutoboa ningumu.

Natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote wa uzi huu (Mwifa, Wizy a.k.a Wkingz mzee wa status๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ na wengine wote) kwa michango yenu .

N.B: Mtoto wa masikini kabisa ametoboa bila connection acha kulalamika inawezekana.
Nilivyofurahi mimi wife amefurahi mara 10 yake๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
Kwa wife nahisi utatafuta mwingine wa type yako!!!๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Nilifanyaga december mwaka jana, bado iko hivyo
Screenshot_20230109-085402~3.jpg
 
Back
Top Bottom